Gwiji wa zamani wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa, Zinadine Zidane ‘Zizou’ amepongeza uteuzi wa kocha wa zamani wa Liverpool Rafael Benitez kukinoa kikosi hicho, lakini amemuonya kuwa lazima ashinde ubingwa wa ligi kuu ‘La Liga’ msimu huu ili awe na maisha mazuri Bernabeu.
Real Madrid hawajashinda kombe hilo la ligi tangu mwaka 2012 walipotwaa wakiwa na kocha wa sasa wa Chelsea, Jose Mourinho.
Rafael Benitez amesaini mkataba wa misimu mitatu kuifundisha timu hiyo akipokea mikoba ya Carlo Ancelloti aliyefukuzwa msimu huu baada ya kushindwa kushinda angalau kikombe kimoja.
Zidane anaamini Benitez anajua kinachotarajiwa kutoka kwake kwenye timu hiyo aliyaonza maisha yake ya ukocha miaka ishirini iliyopita.
“klabu imemsajili Benitez, ni maamuzi mazuri. Lazima kuheshimu uamuzi huo. Benitez ni mwalimu mzuri lakini matokeo ndio kila kitu” Zizou ameliambia gazeti la Marca.
“Anayajua mazingira ya hapa vizuri. Anajua kilichopo mbele yake. Kushinda tu makombe ndio kila kitu hapa.”
Benitez amewahi kutwaa ubingwa huo wa La liga mara mbili akiwa kocha wa Valencia miaka kadhaa iliyopita.
Jina la Zidane lilikua miongoni mwa waliotajwa kurithi mikoba ya kocha Muitaliano Carlo Ancelloti lakini Zizou amesema anahitaji kuendelea kukinoa kikosi cha Madrid Castila ili kupata ujuzi na uzoefu zaidi.
“Imekua ni elimu nzuri. Ni changamoto tofauti na kufundisha kikosi cha kwanza. Tunahitaji kupanda daraja sasa na Real Madrid Castila” anaeleza Zizou “Nimeamua kubaki hapa kwani Madrid ni sehemu nzuri sana nahitaji kuchangia kitu muhimu hapa” amemaliza Kiungo huyo wa zamani wa timu hiyo.