https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    EMANUEL ADEBAYOR ANASEMA UCHAWI NDIO UMESABABISHA AMESHINDWA KUTUPIA NYAVUNI MARA NYINGI MSIMU ULIOPITA


    ade
    Aliwai kupewa jina la AdeMabao wakati anafumania nyavu mara nyingi uwanjani kwenye mechi mbalimbali. Lakini ametupia nyavuni mara chache kupita kiasi ambacho alitegemewa kuisaidia club yake ya Tottenham.

    Ade amesema kwamba mama yake na ndugu zake walikua wanatumia uchawi ili yeye aisiweze kufumania nyavu. Akiwa kwenye interview na radio moja huko Ghana Adebayor amezungumza mambo mbalimbali kuhusu sakata lake na familia yake.
    Mojawapo ni kuhusu yeye kutuhumiwa kumfukuza mama yake kwenye nyumba yake kwa tuhuma za uchawi, Adebayor alijibu “Mimi sio mchungaji, mimi ni mchezaji mpira kwa hiyo siwezi kusema yule ni mchawi. Sijawai kumfukuza kwa sababu ya uchawi aliondoka nyumbani mwenyewe”
    “Nitaanzaje kuwa karibu na mama yangu kama mama huyohuyo ndie anawaambia watu kwamba kazi yangu haitaenda mbele. Inabidi waache kunizungumzia vibaya na waache kushiriki uchawi kwa lengo la kuniharibia mimi. Inabidi waniache nifanya kazi yangu”
    Alindelea kuiambia Peace FM kama hivi ,”Embu fikiria ndugu zako wameshakaa kikao cha kugawana mali kama ukifa wao watagawanaje. Hilo sio swala zuri na wala wakutakiii mema. Eti lile gari litakua lako, ile nyumba itakua yako kama akifa” Adebayor pia alisema anamtumia pesa mama yake kila mwisho wa mwezi.
    Kaka yake Adebayor anaitwa Kola na yeye amesema hivi “Emmanel anaongopewa na wazee flani hivi. Hao ndio wamemwambia kwamba hafungi magoli kwasababu ya uchawi. Wamemwambia dada yake na mama yake wanamfanyia uchwawi ndio maana hafungi magoli. Mama hana furaha na analia kila siku. Nimetoka kumpigia simu na alikua analia pia”
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: EMANUEL ADEBAYOR ANASEMA UCHAWI NDIO UMESABABISHA AMESHINDWA KUTUPIA NYAVUNI MARA NYINGI MSIMU ULIOPITA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top