Wachina na Wajapan wanajulikana kwa vitu vingi sana duniani, wakiwa miongoni mwa nchi zinazo ongoza kwa ubunifu wa Teknolojia duniani.
Nimekutana na stori kutoka Japan ambao wao wamekuja na teknolojia tofauti ya kutoa huduma za hotelini kwa kufungua rasmi hoteli ya kwanza inayoendeshwa na Marobot iitwayo Henn-na Hotel jina ambalo tafsiri yake humaanisha“Hoteli ya ajabu.”
Ukifika
reception utapokelewa na dada huyu, muonekano wake ni wa mwnadamu
halisi, lakini huyu ni mmoja wa Robots waliopo hotelini hapo.
Hoteli ya Henn-na Hotel ipo maeneo ya Huis Ten Bosch Japan na ufikapo hotelini hapo mashine hizo za Robots zitakuwepo reception kukupokea, kukubebea mizigo au kukuhifadhia mizigo yako muhimu sehemu husika yenye ulinzi salama.
Marobot haya yana uwezo ya kuzugumza Kijapan
na wageni wanaofika hotelini hapo na wana uwezo pia wa kupiga stori na
mgeni bila hofu yoyote, wengine kazi yao ni kubeba mizigo ya wageni
hotelini hapo, hoteli hiyo ina vyumba 72 ikiwemo chumba cha
kufulia,kuhifadhia mizigo na chumba cha wafanyakazi.
Hapa chini nimekuwekea video inayo onyesha mashine hizo hapo hotelini
0 comments:
Post a Comment