Penati
ya Alexis Sanchez imewapa Chile ubingwa wa Copa America kwa mara ya
kwanza kwenye mchezo wa fainali kali na ya kusisimua iliyopigwa usiku wa
Jumamosi kati ya wenyeji Chile dhidi ya Argentina na Chile kunyakuwa
kombe hilo kwa penati 4-1.
Ilibidi
mikwaju ya penati iamue nani atanyanyua ndoo hiyo baada ya kushuhudia
dakika 90 za mtanange huo zikimalizika bila timu yoyote kuzifumania
nyavu za mpinzani wake. Zikaongezwa dakika 30 ambazo pia zilimalizika
bila kumpata mbabe wa pambano hilo ndipo mikwaju ya penati ilipotumika
kuamua nani ataondoka na mwali huyo aliyekuwa akigombewa na Mataifa ya
12 ya America Kusini.Mchezo
ulikuwa ni mkali na wa kasi, timu zote zilijitahidi kutengeneza nafasi
na kufanya mashambulizi kadhaa lakini milango yote miwili ilikuwa migumu
kuruhusu nyavu kutikiswa na washambuliaji wa timu zote mbili.
Kombe
hilo linawafanya Chile wamalize ukame wa mataji nchini kwao hasa kwenye
mchezo wa soka kwasababu walikuwa hawajawahi kutwaa taji lolote kubwa
la kimataifa.
Mchezaji nyota wa FC Barcelona
Lionel Messi, ameshindwa kutwaa taji kwa mara nyingine kwenye fainali
yake ya pili akiwa na Argentina baada ya mwaka jana (2014) kulikosa
kombe la dunia mbele ya Ujerumani kwenye fainali za kombe hilo
ilizofanyika nchini Brazil.
Messi ameshashinda mataji yote kwenye ngazi klabu, lakini ameshindwa kutwaa taji lolote akiwa ametinga uzi wa Argentina.
Matias
Fernandez, Arturo Vidal, Charles Arangui na Alexis walifunga mikwaju
yao ya penati wakati wachezaji waliokosa penati kwa upande wa Argentina
ni Gonzalo Higuain ambaye alipaisha juu wakati golikipa wa Chile Claudio
Bravo alipangua mkwaju wa penati uliopigwa na Ever Banega huku Messi
akiwa ni mchezaji pekee aliyefunga penati ya Argentina.
0 comments:
Post a Comment