Mbunge wa Kasulu mjini Moses Machali amesema kuwa yeye na wenzake wanawaachia kazi ya mapambano bungeni wabunge wa UKAWA waliobaki bungeni kuhahakikisha miswada mitatu ya gesi na mafuta haijadiliwi.
Mbunge wa Kasulu mjini Moses Machali amesema kuwa yeye na wenzake wanawaachia kazi ya mapambano bungeni wabunge wa UKAWA waliobaki bungeni kuhahakikisha miswada mitatu ya gesi na mafuta haijadiliwi.
Machali ametoa kauli hiyo katika mahojiano na EATV kufuatia adhabu aliyopewa yeye na wenzake watano ya kutohudhuria vikao vitano vya bunge kutokana na madai ya kuvunja kanuni kwa kumzuia spika kufanya kazi yake.
“Sisi tuliopewa adhabu ndiyo hatutakiwi zaidi, kwahiyo tunawaachia wenzetu wapigane”
Machali amesema hakubaliani na adhabu waliyopewa kwa kuwa utaratibu na kanuni hazikufuatwa wakati wa kusikilizwa
“Kanuni zinasema mtu anapoitwa kuhojiwa anatakiwa kuwa na wakili wake lakini sisi hatujapewa fursa ya kwenda na mawakili……. Mpaka muda huu (saa 3 usiku) hatujaamua nini cha kufanya”
“Kanuni zinasema mtu anapoitwa kuhojiwa anatakiwa kuwa na wakili wake lakini sisi hatujapewa fursa ya kwenda na mawakili……. Mpaka muda huu (saa 3 usiku) hatujaamua nini cha kufanya”
Machali amesema haijawahi kutokea duniani kote miswada mitatu muhimu kama hiyo ikawasilishwa kwa wakati mmoja.
wabunge waliosimamishwa pamoja na Machali ni Pauline Gekul, Tundu Lissu, John Mnyika na Felix Mkosamali.
Ikumbukwe pia Waziri wa Nishati na madini alisema kuwa ni muhimu miswada hiyo ikapitishwa sasa ili kuwahi soko la gesi la dunia.
Katika hatua nyingine mbunge wa Mbozi Magharibi Davidi Silinde amesema seikali ina mpango wa kuwaburuza wabunge kwa kupitisha miswada muhimu kwa taifa kwa muda mfupi bila kuwapa fursa wabunge wausome.

Amesema mapendekezo ya kambi rasmi ya upinzani ni kwamba miswada hiyo iachwe hadi katika bunge la mwezi wa nne ili wananchi na wabunge wapate nafasi ya kuelewa kilichomo.
Silinde amesema kuwa kulazimishwa kwa miswada hiyo ni shinikizo kutoka nchini Marekani kupitia miradi ya MCC.
0 comments:
Post a Comment