Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa alitambulishwa rasmi kuhamia CHADEMA July 28 2015 Dar es Salaam akiwa ameongozana na mke wake, Regina Lowassa pamoja na watoto wao.
Kwenye list ya Viongozi wa UKAWA ambao walikuwepo kumpokea na kumkabidhi kadi ya CHADEMA, alikuwepo James Mbatia, Prof. Lipumba, Dk. Emmanuel Makaidi, Salum Mwalimu na Freeman Mbowe.
Salum Mwalimu ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zanzibar, amesema haya kuhusu mapokezi hayo >>> ‘Tunashukuru
sana Watanzania, sidhani kama kuna kiongozi wa CHADEMA simu yake
iliwahi kuzidiwa kama jana, simu zilizidiwa kwa pongezi… Kila mtu
amezungumza kwa sababu ya Historia ya tendo lenyewe‘>>>>
‘Kesho
Mheshimiwa Edward Ngoyai Lowassa atachukua fomu ya kugombea Urais wa
Tanzania kupitia CHADEMA… pengine kutakuwa na shamrashamra nyingi
itategemeana na Mgombea mwenyewe, akiamua kuja na mdundiko haya… lakini
tunaamini kutakuwa na shamrashamra nyingi‘ >>>> Salum Mwalimu.
Stori zikaanza kuzushwa kuhusu sababu ya Viongozi wengine wa UKAWA kutokuwepo, majibu kayatoa pia Salum Mwalimu>>> ‘Tuna
mambo mengi tuna mikakati mingi, tumegawanyika… sio kila tukio wote
tuwe pamoja, jana mliuliza Tundu Lissu yuko wapi na leo huyu hapa hata
hamumuulizi… Tuko kwenye kipindi cha Uchaguzi tuna mambo mengi hatuwezi
wote kuwa sehemu moja, tunagawanyika kutokana na ratiba tuliyonayo‘>>>>
Sauti ya Salum Mwalimu iko hapa na majibu yote, unaweza kubonyeza play kumsikiliza.
0 comments:
Post a Comment