https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    AZAM YARUDIA REKODI YA BONGE LA KLABU KAGAME

    Azam bingwaTimu ya Azam imechukua kombe la Kagame mwaka 2015 kwa kuifunga Gor Mahia ya Kenya kwa goli 2-0, licha ya kunyakua kombe hilo, Azam imeweka rekodi ya kuchukua kombe hilo bila ya kuruhusu kufungwa goli huku wenyewe wakiwa wametupia wavuni jumla ya magoli 12. Hiyo inakuwa ni mara ya kwanza kwa klabu hiyo kuchukua kombe hilo tangu kuanzishwa kwake miaka tisa iliyopita.
    Mbali na Azam FC, SC Villa ni klabu nyingine ambayo imewahi kutwaa kombe hilo bila kufungwa goli hata moja kama ilivyofanya Azam kwenye michuano ya mwaka huu. Villa ilifanya hivyo miaka 10 iliyopita wakati michuano hiyo ilipofanyika Tanzania pia, kwa hiyo Azam sio timu ya kwanza kuchukua kombe hilo bila kufungwa.
    Azam ilikuwa Kundi C na klabu za KCCA FC, Adama City pamoja na Malakia FC. Azam ilishinda michezo yake yote ya kwenye kundi hilo, Julai 19 ilikutana na KCCA ikashinda kwa goli 1-0 ikiwa ni mchezo wake wa kwanza, Julai 21 ikacheza dhid ya Malakia FC na kuibuka na ushindi wa goli 3-0 kabla haijamaliza mchezo wake wa mwisho wa kundi C kwa kuichapa Adama City kwa goli 5-0 na kuongoza kundi C.
    SC Villa yenyewe ilipangwa kwenye kundi A ambalo lilikuwa na jumla ya timu tano (5) ambazo ni Simba SC, Elman, Rayon Sports na Atletico. Mchezo wa kwanza wa kundi hilo ulikuwa ni April 23, 2005 Villa ilikutana na Simba ambapo Villa ilipata ushindi wa goli 1-0, mechi yake ya pili ilikuwa Aprili 25 Villa ikacheza na Elman na kushinda kwa goli 5-0, Aprili 29 ikatoka sare ya bila kufungana ilipokutana na Rayon Sports na kumaliza mechi za makundi kwa ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Atletico hiyo ilikuwa ni Mei 12005.
    Msimamo wa Kundi A (kundi ambalo ilipangwa SC Villa mwaka 2005)
    1. SC Villa    4  3  1  0  8  0  10  (Uganda)
    2. Rayon Sport   4  2  1  1  7  2    7   (Rwanda)
    3. Simba SC 4  2  1   1  4  2    7  (Tanzania)
    4. Atletico Olympique FC 4  2  1   1  3   9    4  (Burundi)
    5. Elman 4  0  0   4  2  11   0 (Somalia)
    Azam baada ya kuongoza kundi C kwa kushinda mechi zake zote tatu na kutinga hatua ya robo fainali ikiwa imetwaa pointi zote tisa za kwenye kundi lake kwa kuzifunga timu zote, ilikutana na Yanga SC katika hatua ya robo fainali na mchezo huo ukamalizika kwa timu hizo kutoka sare ya bila kufungana na kulazimika kwenda kwenye hatua ya mikwaju ya penati. Yanga ikatupwa nje ya mashindano kwa penati 5-3 na Azam ikasonga mbele kwenye hatua ya nusu fainali.
    Tofauti na ilivyokuwa mwaka huu, mwaka 2005 kulikuwa na makundi mawili ya timu zilizoshiriki michuano ya Kagame na baada ya hatua ya makundi kumalizika hatua iliyofuata ni ya nusu fainali. Hakukuwa na hatua ya robo fainali. SC Villa ikaingia hatua ya nusu fainali na kukutana na Mtibwa Sugar na Villa ikaibuka na ushindi wa goli 1-0 kwenye mchezo wa nusu fainali, hiyo ilikuwa ni Mei 5, 2005. Mpaka hapo Villa ikawa imecheza mchezo wake wa tano bila kuruhusu kufungwa goli.
    Azam wao mchezo wao wa nusu fainali walikutana na KCCA ya Uganda na wakafanikiwa kushinda kwa goli 1-0 lililofungwa na Farid Musa na kutinga hatua ya fainali bila nyavu zao kutikiswa na wapinzani wao waliokutana nao. Lakini wao huo ulikuwa ni mcheo wao watano pia bila kufungwa goli hata moja.
    SC Villa ilikutana na APR FC ya Rwanda kwenye mchezo wa fainali ya michuano ya Kagame uliopigwa Mei 8, 2005 jijini Mwanza na hapo ndipo Villa wakaweka rekodi ya kutwaa kombe la Kagame bila kupoteza mchezo hata mmoja tangu hatua ya makundi hadi mchezo wa fainali.
    Agosti 2, 2015 Azam FC wamerudia kile kilichofanywa na SC Villa kwa kunyakua kombe la Kagame bila kuruhusu kufungwa goli hata moja kwenye michuano hiyo rekodi ambayo imerudiwa wakati mashindano hayo yakifanyika Tanzania.
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: AZAM YARUDIA REKODI YA BONGE LA KLABU KAGAME Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top