https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    CELTIC YATUPWA NJE YA KLABU BINGWA ULAYA, MATOKEO YA MECHI ZOTE YAPO HAPA…

    CelticCeltic imeondoshwa kwenye michuano ya klabu bingwa Ulaya maarufu kama UEFA Champions League kwenye hatua ya kusaka kuingia hatua ya makundi (play-off) baada ya kupigwa kwa wastani wa magoli 4-3 na timu ya Malmo kutoka Sweden.
    Ushindi wa goli 3-2 iliyoupata timu ya Celtic kwenye mechi ya kwanza dhidi ya Malmo ulikuwa mtaji tosha mbele ya wakali hao wa Sweden, lakini wakajikuta wakiangukia pua kwenye mchezo wa jana ambao walikubali kipigo cha goli 2-0.
    Celtic walihitaji ushindi wa goli 1-0 ili kusonga mbele kwenye hatua ya makundi  lakini goli la Nir Bitton alilofunga kwa kichwa lilikataliwa kwasababu kunamadhambi yalitokea kabla ya kufungwa kwa goli hilo.
    Magoli ya jana ya Malmo yamefungwa na Rosenberg katika dakika ya 23 na goli la pili likiwa ni la kujifunga ambapo Dedryck Boyata alijifunga dakika ya 54.
    Matokeo mengine ya michezo ya jana ni kama ifuatavyo;
    Dinamo Zagreb 4-1 Skenderbeu Korce (Aggregate 6-2)
    Maccabi Tel Aviv 1-1 FC Basel (Aggregate 3-3, Maccabi Tel Aviv wanasonga mbele)
    Monaco 2-1 Valencia (Aggregate 3-4)
    Shakhtar Donetsk 2-2 Rapid Wien (Aggregate 3-2)
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: CELTIC YATUPWA NJE YA KLABU BINGWA ULAYA, MATOKEO YA MECHI ZOTE YAPO HAPA… Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top