Mario Balotelli alipigewa picha akiwa kwenye gari lake kabla ya kuingia hospitali kufanya vipimo vya afya na kujiunga rasmi na AC Milan.
Mario Balotelli amejiunga na AC Milan akitokea Liverpool kwa mkopo wa muda mrefu na baada ya kujiunga alisema maneno haya, “Nina furaha nimerejea hapa, nina kidogo tu cha kusema. Binafsi ninategemea kufanya mazoezi ya ziada na kuonyesha thamani yangu. Nipo vizuri kimwili ninachotakiwa ni kufanya mazoezi na timu. Nina vitu vingi vina nipa hali ya kucheza lakini ninachotakiwa ni kucheza soka na sio kuongea.”
Balotelli alifunga magori 26 kwenye mechi 43 akiwa Milan kabla ya kuhama club hiyo.
0 comments:
Post a Comment