https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    MTEULE WA CCM JIMBO LA MBEYA MJINI AKABILIWA NA KESI YA JINAI


    Mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM Mbeya Sambwee Shitambala


    Na Mwandishi wetu,Mbeya

    KESI ya jinai  inayomkabili mgombea ubunge kupitia chama cha mapinduzi Jimbo la Mbeya mjini, Sambwee Shitambala, imeendelea kusikilizwa katika  Mahakama ya Wilaya ya Mbeya.

    Shitambala ambaye ni Mwenyekiti wa zamani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, anatuhumiwa kwa kosa la kuingia kwa jinai baada ya kuvamia na kujenga kwenye eneo la mtu kinyume na sheria katika kiwanja kilichopo eneo la Gombe Jijini hapa.

    Kosa hilo  ni kinyume cha sheria ya 266(a) sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 .

     Akisomewa shitaka hilo na Mwendesha mashitaka wa serikali, Wakili Baraka Mgaya, mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mbeya, Girbelt Ndeuluo, alisema mtuhumiwa alitenda kosa hilo kati ya Juni, 2012 na February 2013 katika eneo la Gombe lililopo Jijini Mbeya
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MTEULE WA CCM JIMBO LA MBEYA MJINI AKABILIWA NA KESI YA JINAI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top