https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    MWANAUME MMOJA AUWAWA KINYAMA HOTELI YA A SQUARE BELMONT ARUSHA


    Mwanaume mmoja ambaye amejulikana jina moja la Reginald, mkazi wa Karatu, amekutwa asubuhi akiwa amefariki, ndani ya hoteli ya A Square Belmont, iliopo katikati ya Jiji la Arusha, huku baadhi ya viungo vyake vya kichwa, sehemu za siri, viganja vya mikono na matiti vikiwa
    havipo na kuachwa kiwili wili kikiwa hakina nguo yoyote.

    Akizungumza leo, katika eneo la hoteli hiyo, Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Levolosi, Sauda Haruna, amesema kuwa yeye alipata taarifa za kifo hicho toka kwa Mjumbe wa serikali ya mtaa Mary Shayo na aliamua kufika eneo la tukio na kukuta kifo hicho cha kusikitisha.

    Sauda ameomba unyama huo usifanyike tena katika Mkoa wa Arusha na wenye hoteli wahakikishe wanaandikisha wageni wao taarifa muhimu, ili kuweza kuwatambua linapotokea tatizo kama hilo.

    Amesema marehemu inakuwa ngumu kufahamu mkazi wa wapi, jina lake kamali kwa sababu hata namba ya simu aliyoandika ikipigwa anapokea mtu mwingine na anashangaa kuulizwa taarifa asizofahamu.

    Kwa upande wake Isike Hamisi, amesema yeye ana ndugu yake alilala katika hotel hiyo jirani na chumba cha marehemu, lakini ahakusikia chochote na asubuhi alishangaa kuambiwa chumba cha jirani kuna mauaji.

    Amesema ni vema hoteli kubwa kama hiyo wafunge kamera za CCTV ili tukio linapotokea inakuwa rahisi kuwafahamu wauaji, tofauti na sasa inavyokuwa ngumu na cha kusikitisha hata damu katika chumba cha marehemu hazikuwepo.

    Kwa upande wa mashuhuda wa eneo la tukio, ambao majina yao hawakutaka kutaja hadharani, wamedai kuwa marehemu huyo anafahamika mkazi wa Mianzini na muuza mabegi, ila jina lililoandikwa katika kitabu hicho sio la kweli.

    Hata hivyo kumpata msemaji wa hotel hiyo haikuwezekana baada ya polisi kusomba wafanyakazi wote, waliopo katika hotel hiyo na kuwapeleka polisi kwa mahojiano zaidi.

    Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha Liberatus Sabas, alipotafutwa kwa njia ya simu, amesema kwa sasa yupo mbali na ofisi na atatoa taarifa hizo baadaye.

    Mwili huo umetolewa katika hotel hiyo majira ya saa 5:45 kupelekwa mochwari na gari la Polisi lenye namba za usajili T.422 AGA, huku umati mkubwa wa watu ukiwa umezingira eneo la tukio.
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MWANAUME MMOJA AUWAWA KINYAMA HOTELI YA A SQUARE BELMONT ARUSHA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top