Arsene Wenger tangu ajiunge na klabu ya
Arsenal mnamo mwaka 1996 amewapa nafasi wachezaji kadhaa kukichezea
kikosi hicho,Petr Cech alikuwa mchezaji wa 199 kuichezea Arsenal mchezo
wa kwanza akiwa chini Wenger,katika kipindi hicho chote
kama mshambuliaji kinda Alex Iwobi
angepewa nafasi ya kucheza hapo jana kwenye mchezo dhidi ya Chelsea basi
angekuwa mchezaji wa 200.
kikosi cha kwanza cha Wenger mara tu baada
ya kujiunga Arsenal kilikuwa na nyota kama vile David Seaman, Tony
Adams, Ian Wright na Martin Keown,kikosi hicho kilishinda mabao 2-0
dhidi ya Blackburn.
Mchezaji mgeni wa kwanza kuicghezea
Arsenal chini ya Wenger alikuwa Patrick Vieira, Mfaransa wa kwanza kati
ya 26 walioichezea Arsenal katika kipindi cha utawala wa Wenger.
Wachezaji wafuatao namba zao kwenye mabano ni miongoni mwa wanandinga
walioichezea timu iyo kwenye utawala wa Wenger,Dennis Bergkamp (13th),
Thierry Henry ( 48th),Alexis Sanchez (193), Mesut Ozil (183),Santi
Cazorla (173),
Tomas Danilevicius (65),Patrick Cregg (106).
Hii ndio orodha ya wachezaji wote waliofanikiwa kuichezea Arsenal chini ya utawala wa Arsene Wenger.
0 comments:
Post a Comment