MKURUGENZI
wa Huduma na Uendeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ya Jamii
Tanzania, NHIF, Eugine Mikongoti, akiwasilisha mada juu ya mpango wa
uchangiaji binafsi, KIKOA, wakati wa warsha ya siku moja iliyoandaliwa
kwa pamoja kati ya NHIF, na Mtandao wa Bloggers Tanzania, TBN, na
kufanyika kwenye ukubmi wa Baraza la Maaskofu Tanzania, Kurasini jijini
Dar es Salaam, Agosti 13, 2015
NA K-VIS MEDIA
MFUKO
wa Taifa wa Bima ya Afya ya Jamii Nchini Tanzania, NHIF, umekutana na
wanachama wa chama cha waandishi wa habari wa mtandao (TBN), na kuwapa
elimu juu ya mpango wa uchagiaji wa “KIKOA”, ambao unahusu watu binafsi
walio kwenye vikundi.
Akitoa
mada juu ya mpango huo, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko huo
anayesimamia mpango wa uchagiaji binafsi, (KIKOA), Eugine Mikongoti,
amesema, mfuko wa bima ya afya chini ya sheria ya kuanzishwa kwa mfuko
huo, sheria namba 8 ya mwaka 1999, ni kusimamia upatikanaji wa huduma za
kimatibabu kwa wananchi kwa utaratibu wa kuchagia kabla ya kuugua na
kupata matibabu kupitia Hospitali za Serikali, Madhehebu ya dini, zan
Binafsi na Maduka ya Dawa ambayo yamesajiliwa.
Alisema,
mwanachama wa KIKOA atachangia shilingi 76, 800/- kwa mwaka na
atapatiwa kadi ya matibabu ya NHIF ambayo ataitumia kupata matibabu
katika vituo zaidi ya 6,000 vilivyosajiliwa na NHIF nchi nzima.
Pia
alisema, Mwanachama wa KIKOA anayo fursa ya kuwaingiza mwenza wake na
nafasi nne kwa ajili ya watoto (miaka 18 hadi 21) kama bado wanasoma na
wazazi wake na wazazi wa mwenza wake, kwa utaratibu ule ule ya kuwalipia
kila mmoja shilingi 76,800/- kwa mwaka kwa kila mmoja
Mgeni rasmi Mkurugenzi
wa Masoko na Utafiti wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii ya Tanzania,
NHIF, Rehami Athumani, akifungua warsha hiyo. Kushoto ni Katibu Mkuu wa
TBN, Khadija Kalili
Baadhi ya washiriki wa warsha hiyo, wakifuatilia kwa makini
Rehani Athumani
Bloggers kutoka Bagamoyo
Bloggers wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa








0 comments:
Post a Comment