Waziri wa Uchukuzi Samwel Sitta akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya kuchukua hatua kubwa kuanza kufufua reli ya kati muda wowote, ujenzi wa reli hiyo utaanza ili kuongeza kasi ya maendeleo hapa nchini leo Jiji Dar es Salaam.
Waandishi wa habari walio hudhulia katika mkutano na Waziri wa Uchukuzi Samwel Sitta, wakimsikiliza kwa makini.
(Picha na Emmanuel Mssaka.
Na JenikisaNdile –Maelezo
SERIKALI kwa kushirikiana na kampuni ya reli Asset holding imejizatiti kuimarisha miundo mbinu ya reli itakayogharimu Tsh. Trilioni 16 katika kuleta maendeleo endelevu hapa nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam waziri wa uchukuzi Mhe. Samweli sitta amesema kuwa mkakati ni kuimarisha reli katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Aliongeza kuwa maeneo yatakayonufaika na uboreshwaji wa miundo mbinu hiyo ni pamoja na Songa Mpiji. Mtwara hadi Mbambabay, Songea hadi Mchuchuma na mradi mpya wa reli ya kutoka Dar es Salaam hadi Bagamoyo.
“Lengo la miradi hii ni kuhakikisha kuwa tunaleta maendeleo ya kiuchumi kwa kujipatia fedha za kigeni ambazo zitatokana na usafirishaji wa mizigo nje ya nchi “ amesema Mhe. Sitta.
Aliongeza kuwa miradi hiyo inatarajiwa kuanza mwanzoni mwa mwezi wa tisa ambapo Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Jakaya Kikwete ataweka jiwe la msingi tayari kwa utekelezaji.
Aidha alibainisha kuwa kwa kuimarisha miundo mbinu ya reli kutasaidia katika kurahisisha usafirishaji wa mizigo yenye uzito mkubwa kama mafuta, makaa ya mawe na chuma ndani na nje ya nchi.
0 comments:
Post a Comment