Salym Juma
Asalam aleykum wapenzi wa michezo popote mnapoisoma Makala hii, naamini hali zenu ni nzuri na mnaendelea vyema na shughuli zenu za kila siku. Baada ya kuwa bize na habari za siasa ambazo ndizo zinasumbua vichwa vya watu kibao, naomba sasa utulie na uburudike na habari moto moto za kimichezo katika ukurasa huu ambao pengine ndio unaoongoza kwa kusomwa na wapenzi wengi wa soka nchini Tanzania.
Kila binadamu mpenzi wa soka lazima ana timu anayoipenda kwa dhati, huwezi kuwa mpenda soka alafu ukakosa timu ya kuishabikia, bila shaka wewe utakuwa ‘Lofa’ kama sio Mnafiki. Mimi binafsi mbali na kuipenda
timu yangu ya nyumbani ya AFC ya hapa Arusha, pia ni shabiki wa kutupwa wa Borussia Dortmund na ninaumia sana tunapoonewa na wale wekundu wa Munich, anyway waamuzi wa soka pale EPL pia wamekuwa
wakichezesha mechi kibao ila nao kama binadamu na wapenzi wa soka wana vilabu vyao.

Leo hii naomba upoteze muda wako kutazama baadhi ya waamuzi na taaluma zao nje ya uwanja huku nikikuwekea pia na timu wanazozipenda kutoka moyoni licha ya kufanya kazi za Uamuzi, karibu sana tafadhali.
MARK CLATTENBURG- SHABIKI WA KUTUPWA WA NEWCASTLE UNITED
Ni mwamuzi mwenye miaka 40 na anakuwa miongoni mwa waamuzi wadogo kabisa kwenye EPL. Ndani ya misimu mitatu iliyopita amesha chezesha mechi 75 na kutoa kadi za njano 258 huku nyekundu zikiwa 11. Alianza kazi yake akiwa na miaka 25, nadhani wengi tutamkumbuka kwa ile kashfa ya kumbagua Mikel Obi kwenye mechi ya EPL japokuwa baadae alikutwa hana hatia. Aliweka rekodi kwa kuwa mwamuzi mdogo kuchezesha mechi za FIFA, hapa alikuwa na miaka 30.
Kitaaluma huyu mwamuzi ni Mwanasheria ila hapo awali alikuwa ni fundi umeme. Kama alivyo mwanadamu mwingine, Clattenburg pia ana hisia na kuguswa na timu fulani. Hapa nazungumzia mapenzi yake kwenye timu ya Newcastle Unted. Mwamuzi huyu amekuwa akiguswa na uchezaji wa Newcastle tangu siku nyingi na amekiri mara kadhaa.
MARTIN ATKINSON- SHABIKI WA KWELI WA LEEDS UNITED
Huyu jamaa ana miaka 44 na alianza kazi ya uamuzi pindi akiwa na miaka 16, kazi hii aliianza baada ya kutokuwepo kwa waamuzi kwenye mechi za mtaani kwake. Tunamfahamu zaidi kwa uamuzi wake wa furaha kwani jamaa anaweza kukupa kadi huku anacheka. Hadi sasa ndani ya misimu mitatu iliyopita Martin amechezesha mechi 82 na kutoa kadi za njano 294 huku kadi nyekundu zikiwa 11. Amesha chezesha mechi kubwa sana katika ngazi zote za vilabu barani Ulaya.
Kitaaluma huyu jamaa ni Polisi, ndiyo nakwambia ni afisa wa Polisi sasa unashangaa nini..! Japokuwa alionekana kuipendelea Man U, ila huyu jamaa ni mpenzi na shabiki mkubwa wa Leeds United ya pale
Uingereza. Amekuwa akivurunda mara kibao na pia mara chache ameomba radhi kwa madudu yake uwanjani.
Uingereza. Amekuwa akivurunda mara kibao na pia mara chache ameomba radhi kwa madudu yake uwanjani.
ANTHONY TAYLOR- SHABIKI WA KUFA WA ALTRINGHAM FC
Japokuwa ana miaka 36, ila alianza kazi ya uamuzi muda mrefu sana tangu wakati Rais mkapa anaingia madarakani. Kaanza kazi siku nyingi sana ila alipandishwa kuchezesha ligi kuu mwaka 2010 kwani muda mwingi alikuwa anachezesha mechi za madaraja ya chini huko Uingereza. Ndani ya misimu mitatu iliyopita ameshachezesha mechi 74 na kumwaga kadi 237 huku akitoa kadi nyekundu 13 pekee. Taylor amekuwa miongoni mwa waamuzi wanaolalamikiwa mara kwa mara.
Taaluma yake ni bwana jela. Eeeh, bwana jela ndiyo sasa unashangaa kitu gani..! Mbali na kufanya kazi na wafungwa, pia huyu jamaa ni shabiki wa kufa wa timu ya Altringham FC, timu kongwe inayopatika huko
Manchester na inashiriki madaraja ya chini. Watu wengi tunamkumbuka zaidi alipovurunda mechi ya Arsenal na Aston Villa mwaka 2013.
Manchester na inashiriki madaraja ya chini. Watu wengi tunamkumbuka zaidi alipovurunda mechi ya Arsenal na Aston Villa mwaka 2013.
MIKE DEAN- SHABIKI HATARI WA TRANMERE ROVERS.
Ni miongoni mwa waamuzi wakongwe kabisa barani Ulaya na nchini Uingereza akiwa na miaka 47 hadi sasa. Mike anadai yeye ni mkongwe kwenye fani hii kwani ana miaka 30 tangu aanze kuchezesha mechi za
soka. Ukijaribu kuangalia misimu mitatu iliyopita, Mike amechezesha mechi 84 huku akimwaga kadi za njano kama njugu kwa kutoa jumla ya kadi 322 na zile nyekundu 15 pia. Mike alitajwa mara kadhaa kustaafu tangu
akiwa na miaka 45 ila cha ajabu bado yupo dimbani.

Japokuwa taaluma yake amekuwa akiificha, ila ukweli ni kwamba Mike ni shabiki wa kufa wa Tranmere Rovers. Timu hii ni kongwe sana kwani ina miaka mingi na imekuwa ikishiriki madaraja ya chini ya ligi za
Uingereza. Anakumbukwa zaidi kwa kumuogopa Ferguson kwani mwaka 2010 aliwanyima Chelsea penati 4 Old Trafford.
Uingereza. Anakumbukwa zaidi kwa kumuogopa Ferguson kwani mwaka 2010 aliwanyima Chelsea penati 4 Old Trafford.
MICHAEL OLIVER- SHABIKI WA KUTUPWA WA NEWCASTLE UNITED.
Ni mwamuzi mdogo pengine kuliko wote kwa sasa katika ligi kuu ya Uingereza. Oliver ana miaka 30 pekee na ameanza kazi yake tangu akiwa na miaka 14. Bwana mdogo huyu amekuwa gumzo sana kwani ndani ya misimu mitatu iliyopita, ameshachezesha mechi 77 na kutoa kadi za njano 248 huku zile nyekundu zikiwa 8. Anashikilia rekodi ya kuwa mwamuzi mdogo kuchezesha EPL akiwa na miaka 25 mwaka 2010. Bila shaka unamfahamu zaidi huyu jamaa kwani tushaandika Makala sana kumuhusu.
Nje ya uwanja huyu Jamaa anafanya kazi ya kuratibu waamuzi kwenye akademi inayofunza waamuzi. Pia ni shabiki wa kutupwa wa Newcastle na hii inachagizwa na kukulia kwake karibu na timu hii. Bila shaka wengi
wanamkumbuka kwenye mechi ya Chelsea na Swansea na alivyompa Di Maria
kadi nyekundu.
wanamkumbuka kwenye mechi ya Chelsea na Swansea na alivyompa Di Maria
kadi nyekundu.
LEE MASON- MNAZI WA BOLTON WANDERERS
Ni Babu Fulani mwenye kipara na mwaka huu anatimiza miaka 43 tangu kuzaliwa kwake. Ni miongoni mwa waamuzi wachache walioanza kazi kabla hata Michael Oliver hajazaliwa..! Ana wastani wa kutoa kadi tatu za njano kwa kila mechi kwani tayari ametoa kadi 225 ndani ya mechi 73 hadi
sasa huku akiwa na kadi 12 nyekundu katika vitabu vya rekodi. Mwaka 2006 Mason alichezesha mechi yake ya kwanza ya EPL na baada ya hapo amekuwa na mwendelezo wa kuchezesha mechi kibao.
sasa huku akiwa na kadi 12 nyekundu katika vitabu vya rekodi. Mwaka 2006 Mason alichezesha mechi yake ya kwanza ya EPL na baada ya hapo amekuwa na mwendelezo wa kuchezesha mechi kibao.
Nje ya soka, Lee Mason ni Mfanyabiashara na kabla ya hapo alikuwa ni mkusanya kodi nchini Uingereza. Kama walivyo binadamu wengine, Masoni pia ana mapenzi na timu fulani, timu hii siyo nyingine bali ni Bolton
Wanderers. Mwamuzi huyu anakumbukwa kwa kuwaonea Chelsea mwaka 2012 pale alipowatoa nje Torres na Ivanovic huku akiwanyima Blues penati kadhaa pale Old Trafford.
Wanderers. Mwamuzi huyu anakumbukwa kwa kuwaonea Chelsea mwaka 2012 pale alipowatoa nje Torres na Ivanovic huku akiwanyima Blues penati kadhaa pale Old Trafford.

0 comments:
Post a Comment