Ukiwa ndani ya ndege unasafiri kuna wale wahudumu ambao wanakuwa wanazunguka hivi kuhudumia wasafiri, muda mwingi ni wakarimu na utaona wanatabasamu muda wote, unadhani hawapumziki?
Nimekutana na story kwenye mitandao mikubwa Duniani, wamesapoti kabisa story yao kwa ushahidi wa pichaz kwamba kama ukiona wahudumu hawaonekani katikati ya safari, wakati mwingine wanakuwa wamelala.. unajua vyumba viliko?
Ndani ya ndege nyingi kubwa kama Boeing 777 au 787 ambazo zinafanya safari ndefu kama kutoka Amsterdam Uholanzi mpaka New York Marekani ndani kuna hivi vyumba vya wale wahudumu kupumzika wakiwa safarini.
Unaambiwa kwenye ndege nyingine mlango ni wa siri kabisa, huu unafunguka kwa juu kama sehemu ambayo inawekwa mizigo kwa juu ndani ya ndege.
Kwenye ndege nyingine vitanda vya wahudumu viko juu, hii ni ramani yake, watu wanaendelea na safari kwa chini alafu wahudumu wanakuwa wamepumzika zao kwa juu.


0 comments:
Post a Comment