Viungo washambuliaji wa klabu ya arsenal ya jijini London, Theo
Walcott na Santiago Cazorla wamesaini mikataba mipya itakayowakikishia
kubaki pale Emirates.
Theo Walcott ambaye amefunga magoli 76 katika mechi 302 akiwa na
washika bunduki alijiunga na klabu hiyo akitokea pale Saint marry
mwaka 2006. Amesaini mkataba wa miaka 4 na atakuwa analipwa kitita cha
Euro 140, 000 kwa wiki na kuwa miongoni mwa wachezaji wanaolipwa
mishahara ya juu pale Emirates.
Mchezaj huyo mwenye miaka 26 alimaliza msimu kwa staili nzuri baada
ya kupiga “hatrick” kwenye mechi ya mwisho dhidi ya West Brom, pia
alifunga kwenye ushindi mnono wa magoli 4 dhidi ya Aston Villa kwenye
fainali ya FA.
Pia kiungo matata kutoka Hispania, Santiago Cazorla mwenye miaka 30
pia amesaini mkataba wa miaka 2. Cazorla amecheza mechi 148 tangu
ajiunge na Arsenal kutoka Malaga huku akifunga magoli 27 likiwemo goli
la fainali ya FA mwaka 2014.
Inawezekana mikataba hii ikazidi kuwanufaisha arsenal, kwani wachezajihawa ni muhimu sana katika kikosi cha Wenger ambacho kinatarajiwa
kutwaa ubingwa msimu ujao wa EPL
0 comments:
Post a Comment