https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

.

.

.
  • Latest News

    .

    Watoto watano wa mastaa wa soka waliofuata nyayo za baba zao, picha & video zipo hapa

    Mwaka 2012 kocha wa Arsenal, Arsene Wenger alikuwa wa kwanza kuomba kumsajili mtoto wa Lionel Messi ili akikua ajiunge na Academy ya Arsenal, hiyo inaonesha pia kwamba kuna watoto wengi wa wanasoka hupewa nafasi kubwa ya kufuata nyayo za baba zao.
    Nimekusogezea picha na video za watoto wa mastaa waliofuata nyayo za baba zao.
    1. Enzo Zidane ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Ufaransa na klabu ya Real Madrdid ya Hispania Zinedine Zidane... Enzo amefuata  nyayo za baba yake na hivi sasa yupo katika timu ya vijana ya Real Madrid. Enzo ni mjanja na anajua kuuchezea vizuri mpira kama baba yake.
    1416316096_extras_noticia_foton_7_1
    Enzo na baba yake Zidane

    2. Rivaldinho ni mtoto wa  Rivaldo staa wa soka kutokea Brazil lakini pia amewahi kuichezea FC Barcelona ya Hispania kwa mafanikio, Rivaldinho amefuata nyayo za baba yake kwa kuanza kuichezea klabu iliyomlea baba ya Mogi Mirim na kwa sasa wanacheza pamoja na baba yake katika klabu hiyo.
    download
    Rivaldo na mtoto wake Rivaldinho

    3. Tom Ince ni mtoto wa staa wa zamani wa Uingereza Paul Ince ambae amewahi kutamba katika vilabu vya West Ham United, Manchester United na Liverpool ila Tom anachangamoto kubwa ya kupata mafanikio kama aliyofikia baba yake. Tom Ince kwa sasa anaichezea Derby County.
    incethomas_ince-42_1701866a
    Paul Ince na mtoto wake Tom

    4. Justin Kluivert yupo katika Academy ya Ajax  Uholanzi baba yake Patrick Kluivert amewahi kutamba katika klabu ya FC Barcelona na timu ya taifa ya Uholanzi.
    7
    Justin Kluivert na baba yake Patrick Kluivert

    5. Joe van der Sar ni mtoto wa golikipa wa zamani wa Manchester United Edwin van der Sar, amefuata nyayo za baba yake si kwa kucheza soka tu bali hata nafasi anayoichezea ni sawa na baba yake. Joe yupo katika Academy ya Ajax.
    Edwin Van der Sar (R),son Joe (L) during the Edwin van der Sar Testimonial match at the Amsterdam Arena on August 3, 2011 in Amsterdam, Netherlands. (Photo by VI Images via Getty Images)
    Joe na baba yake Edwin van der sar

    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Watoto watano wa mastaa wa soka waliofuata nyayo za baba zao, picha & video zipo hapa Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top