Nyota wa soka Angel di Maria
amekosoa filosofia ya kocha wa Manchester United Louis Van Gaal na
kudai kuwa alikorofishana na kocha huyo Mdachi.
Kiungo huyo wa Argentine alijunga na
Manchester United kwa rekodi ya kitita cha paundi milioni 60 Agosti
2014 alishindwa kuzoea mazingira ya Old Trafford na kuhamia timu ya
Paris Saint-Germain mapema mwezi huu.
Di Maria amesema ilikuwa vigumu
kwake kuweza kuiva na Van Gaal ambaye ni mkorofi, jambo ambalo
lilimfanya asijisikie vizuri kufanya kazi za kocha huyo wa Manchester
United.
0 comments:
Post a Comment