https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    BALOZI SEIF AFANYA MKUTANO NA WANA CCM WA KIJIJI CHA KWALE WILAYA YA MICHEWENI


    Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
    amewatahadharisha Wananchi kuwa makini na Watu wanaochochea chuki
    miongoni mwa Jamii jambo ambalo  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
    kamwe haitakubali kuona amani ya Nchi inachezewa kizembe.
     
    Alisema wapo watu waliochoka na amani iliyopo nchini kwa kuanza
    kushabikia cheche za kujiandaa kuwashawishi Vijana wawe tayari kufanya
    fujo mara tuu baada  ya zoezi la kupiga kura kwenya uchaguzi Mkuu wa
    Mwezi Oktoba mwaka huu.
     
    Balozi Seif Ali Iddi ametoa tahadhari hiyo wakati akizungumza na
    Wananchi pamoja na Wana  CCM wa Kijiji cha Kwale Wilaya ya Micheweni
    Mkoa wa Kaskazini Pemba akitekeleza ahadi aliyowapa wazee wa Kijiji
    hicho hivi karibuni ya kuwatembelea na kusalimiana nao.
     
    Balozi Seif aliwaonya Vijana kujiepuka na mtego huo ulioandaliwa kwa
    ajili yao unaoweza kuwaathiri na akawatolea mfano wa matukio ya
    Januari mwaka 2001 ambayo waandaji wakubwa waliwazuia Vijana wao na
    kuwaachia Vijana wa wenzao kutumbukia katika balaa.
     
    Akizungumzia Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika siku 49 zijazo
    Balozi Seif ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya
    Taifa ya CCM aliwakumbusha wana CCM na Wananachi hao wa Kijiji cha
    Kwale kuendelea kuiunga mkono CCM ibakie madarakani.
     
    Alisema Dira ya Cahama cha Mapinduzi ni kuwanuganisha Wananachi wote
    katika kudumisha Umoja na Mshikamano kwani tabia ya mfarakano
    inayoonekana kubebwa na upinzani imepigwa vita hata katika vitabu wa
    Dini.
     
    Balozi Seif amewapa pole Wananchi wa Kijiji hicho cha Kwale kutokana
    na madhila waliyoyapata kufuatia kitendo cha Upinzani kutaka kupachika
    Bendera kwa nguvu ndani ya Kijiji hicho bila ya ridhaa ya Wananchi
    wenyewe.
     
    Alisema Wanachama wa Chama cha Mapinduzi kamwe hawakubali kuonewa na
    Uongozi wa Chama hicho katika ngazi zote daima utaendelea kutetea
    maslahi yake muda wowote ule.
     
    Katika Mkutano huo Balozi Seif Ali Iddi alipata fursa ya kuizindua
    rasmi Maskani ya Chama cha Mapinduzi ya Wazede wa Kijiji hicho cha
    Kwale kiliomo ndani ya Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.

    Othman Khamis Ame
    Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: BALOZI SEIF AFANYA MKUTANO NA WANA CCM WA KIJIJI CHA KWALE WILAYA YA MICHEWENI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top