ZOEZI LA KUGAWA CHAKULA LAENDELEA KATIKA KAMBI YA WAKIMBIZI YA NYARUGUSU ILIYOKO WILAYANI KASULU MKOANI KIGOMA
Wakimbizi
kutoka nchini Burundi walioko katika kambi ya Nyarugusu wakiwa wamebeba
shehena ya unga wa mahindi jana, muda mfupi baada ya kugawiwa chakula
hicho Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia chakula (WFP),
lililoweka kituo chake katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu wilayani
Kasulu, mkoaniKigoma.
Byesige
Josephat (anayemimina mafuta) na Hezron Mtangirwa (kushoto), wakimbizi
kutoka Burundi waliohifadhiwa katika kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu
wakipima mafuta ili waweze kuyagawa kwa wakimbizi wenzao jana,baada ya
kugawiwa mafuta na Shirika la Umoja wa Mataifa, linaloshughulikia
chakula (WFP), ambalo lina kituo chake katika kambi ya Nyarugusu iliyoko
wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
Kina
mama wa kimbizi toka Burundi wakipata mgao wao wa unga unaotolewa kwa
wakimbizi wanaohifadhiwa katika Kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko
wilayani Kasulu mkoani Kigoma. Serikali kwakushirikiana na Mashirika ya
Kimataifa imeendelea kuhakikisha kuwa wakimbizi hawa toka Burundi
wanapata chakula cha kutosha kwaajili ya mahitaji yao.
Mkimbizi Irene Ntibelenda (katikati) akiwa pamoja na ndugu yake Sengiyu Mvajeme (kulia) wakiwa wamebeba mgao wa chakula.
Wakimbizi wakifunga shehena ya mahindi.
Sehemu ya shehena ya chakula ukiwepo unga wa mahindi na mafuta ya kupikia ikiwa katika ghala la kuhifadhia chakula.
Item Reviewed: ZOEZI LA KUGAWA CHAKULA LAENDELEA KATIKA KAMBI YA WAKIMBIZI YA NYARUGUSU ILIYOKO WILAYANI KASULU MKOANI KIGOMA
Rating: 5
Reviewed By: Unknown
0 comments:
Post a Comment