Kocha ambae kibarua chake kimeota nyasi kutoka Real Madrid amefanya interview na gazeti la Marca kuhusu mambo mbalimbali. Kati ya maswali ambayo yaliteka sana watu ni kutaka kujua kwa mawazo yake nani ataibuka kuwa mfungaji bora msimu huu kati ya CR7 na Messi.
Jibu lake lilikua hivi, “Sina wasiwasi na Cristiano Ronaldo licha ya kushindwa kutupia nyavuni kwenye mechi mbili za mwanzo wa msimu. Najua Cristiano yupo vizuri na kama ingekua kucheza kamali ningeweka pesa zangu kwake kama mfungaji bora wa msimu huu.Jibu langu ni Cristiano Ronaldo na ligi ya Hispania ina bahati ya kuwa nao wote wawili”
Sasa kwa mawazo yako wewe unadhani nani atakua mfungaji bora kwa msimu ujao kati ya hawa wawili?


0 comments:
Post a Comment