Wachezaji wa Azam FC wakiwa wamembeba kocha wao juujuu wakishangilia ushindi wa Kagame
Jana timu ya Azam FC ilibeba kombe la Kagame kwa mara kwanza kwenye historia ya timu hiyo tangu kuanzishwa kwake. Wachezaji, makocha na viongozi wengine wa timu hiyo walikuwa ni wenye furaha sana baada ya kukabidhiwa kombe hilo.
hizi ni picha zikionesha jinsi walivyofurahia kunyakua ubingwa huo kwa kuifunga timu ya Gor Mahia ya Kenya kwa goli 2-0.
Wachezaji wa Azam FC kwapamoja wakiwa wamelibeba kombe la Kagame
Kocha wa Azam fc Stewart Hall akiwa pamoja na wachezaji wake kwenye picha ya pamoja mara baada ya kutwaa ubingwa wa Kagame
Wachezji na viongozi wa Azam wakishangilia ushindi kwa pamoja
Beki wa Azam FC Agrey Morris akiwa amembeba mtoto wake muda mfupi baada ya pambano la fainali kumalizika
Wachezaji wa Azam wakipita kuwashukuru kwa kuwapigia makofi mashabiki walijitokeza kuwashangilia kwenye mchezo wa fainali mara baada ya mchezo kumalizika
Kikosi kizima cha timu ya Azam FC kikiwa kinashangilia ubingwa wa Kagame
Mashabiki wa timu ya Azam FC wakiwa wameshika T-Shirt iliyoandikwa maneno ya kumsifia nahoha wa kikosi chao John Bocco ‘Adebayor’A
0 comments:
Post a Comment