Staili ya mchezo wa kushambulia ya klabu ya Manchester United imekuwa
ikishambuliwa na wachambuzi wa michezo msimu huu lakini hakukuwa na
mashaka juu ya ubora wa pasi 45 zilizopigwa kabla ya kufungwa kwa goli
la tatu dhidi ya Southampton..

Goli hilo Juan Mata lilihakikishia United ushindi muhimu lakini pia
limewezq kuingia katika listi ya magoli yaliyofungwa baada ya kupigwa
kwa pasi nyingi katika kipindi cha miaka 5 iliyopita ndani ya Barclays
Premier League.

Kabla
ya kufungwa kwa goli hilo Manchester United walipiga pasi 45, na hivyo
kulifanya goli hilo kushika nafasi ya pili – kwa idadi ya pasi kabla ya
goli – huku nafasi ya kwanza ikishikwa na goli la Nacer Chadli wa
Tottenham aliyefunga goli dhidi ya QPR baada ya kupigwa kwa pasi 48.
Chadli alifunga goli hilo katika mechi ya raundi ya kwanza ya EPL msimu uliopita.
Listi ya magoli ya magoli yaliyofungwa baada ya namba kubwa ya pasi katika EPL
0 comments:
Post a Comment