https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    Hili ndio Oven la computer ambalo halihitaji mpishi wala maelekezo! + (Video).

    Kama kungekuwa na uwezo wa kutumia Computer kupika chakula maisha yangekuaje? Au kama simu yako ingekuwa na uwezo wa kupokea ujumbe wa kukutaarifu kuwa chakula chako kipo tayari maisha yangekuaje!?
    Nimekutana na stori kutoka Marekani ambako Matt Van Horn na rafiki yake Nikhil Bhogal wametengeneza computer waliyoipa jina ‘June Intelligent Oven’.
    june8
    June ni oven ya computer inayofikiria na kufanya kazi kama mpishi ‘chef’, oven hiyo inayopatikana kwa dola 1,495 (Million 3,289,000) inatumia computer kutambua ni aina gani ya chakula unataka kupika na kukuelekeza jinsi ya kukipika vizuri zaidi.
    >>“hili oven lina uwezo wa kufanya kazi kama computer, simu au hata tablet… kwa uraisi na ufupi ‘June’ ni computer yenye uwezo wa kupika chakula chochote bila msaidizi au mpishi”.<<< Matt Von Horn.
    mat von
    Matt na Nikhil ndio wabunifu wa teknolojia hii ya June Intelligent Oven.
    Hili oven halhitaji kuwashwa ili likolee moto lenyewe hufanya kazi kama vile computer nyingine na kizuri zaidi ni kwamba kwa kutumia application yake ya simu iitwayo ‘June Application’ hili oven lina uwezo wa kutuma ujumbe mfupi kwenye simu yako kukutaarifu  pale chakula chako kikiwa tayari!
    june7
    Ni mwaka jana tu ambapo Matt na Nikhil waliamua kuacha kazi zao ili kuifanyia kazi ndoto hii, na mwezi uliopita June Intelligent Oven ilizinduliwa rasmi lakini jiko hilo litaanza kusafirishwa mwanzo wa mwaka ujao.
    Hizi ni baadhi ya picha za oven la June nilizoweza kuzinasa..
    june
    June Intelligent Oven.
    june2
    June Intelligent Oven lina uwezo wa kukuonyesha moja kwa moja kwenye simu yako dakika ngapi zimebaki chakula chako kiive.
    june3
    Oven hii pia inauwezo wa kupandisha na kushusha joto na moto lenyewe na kukuonyehsa kila kitu kwenye simu yako.
    june5
    Unaweza ukaangalia jinsi chakula kinavyoiva kwa kupitia camera ya oven hiyo kwenda moja kwa moja kwenye simu yako.
    june7
    Chakula kikiwa tayari au kikikaribia kuiva… oven hii inakutumia ujumbe mtu wangu.
    june4
    Pale tu unapoweka chakula chako oven hii inauwezo wa kusoma na kujua moja kwa moja unataka kupika nini na kukushauri jinsi ya kukipika.
    june
    Kama ikitokea hujui cha kupika, kwa kutumia application ya ‘June App’ kwenye simu au tablet yako, Oven hiyo itakupa orodha ya vyakula vya kuchagua.
    Na hapa chini nimekusogezea video yake ikielezea jinsi ya kutumia oven hio kwa kutumia simu au tablet yako mtu wangu.
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Hili ndio Oven la computer ambalo halihitaji mpishi wala maelekezo! + (Video). Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top