Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais
Mazingira, Dk.Binilith Mahenge (kulia), akikata utepe kuashiria uzinduzi
wa kituo cha oparesheni cha Kampuni ya MagilaTech, iliyotengeneza
teknolojia ya tigo backup inayowezesha kurejesha kumbukumbu na kuzuia
wizi wa simu za mkononi Dar es Salaam leo.
Wanahabari na wadau wengine wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa DTBi, Mhandisi George Mulamula (kulia), akizungumza katika uzinduzi huo.Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez (kulia), akitoa hutuba yake.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk. Hassan Mshinda (kulia), akizungumza katika uzinduzi huo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya DBTi, Balozi Ami Mpungwe.
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Dk.Binilith Mahenge, kwa niaba ya Makamu wa Rais Dk.Mohammed Gharib Bilal aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo akisoma hutuba.
Meneja wa mradi huo kutoka Tigo,
Atuletye Mwamila (kulia), akielekeza jinsi teknolojia hiyo inavyofanya
kazi na kuwezesha kuipata simu iliyopotea na kumbukumbu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Magila Tech iliyotengeneza Teknolojia ya Tigo Backup, Godfrey Magila akielezea jinsi teknolojia hiyo inavyofanya kazi.
Mwenyekiti wa Bodi ya DBTi, Balozi
Ami Mpungwe (kushoto), akizungumza katika uzinduzi huo. Kulia ni
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk.
Hassan Mshinda.
Wanahabari wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Maofisa wa ufundi, Rahim Hussen
(kushoto) na Mkupete Mkamba (kulia), wakitoa maelezo wa kifaa mfano wa
ndege kinachorushwa angani na kuweza kubaini magonjwa katika mimea
walicho kibuni.
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Dk. Binilith Mahenge (katikati),
akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kituo cha oparesheni cha Kampuni
ya Magila Tech, iliyotengeneza teknolojia ya tigo backup inayowezesha
kurejesha kumbukumbu na kuzuia wizi wa simu za mkononi Dar es Salaam
leo, kilichopo Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech). Kituo
hicho kinashirikiana na kampuni ya simu ya tigo, Dar Teknohama Business
Incubator (DTBi), pamoja na Costech kuendesha mradi huo. Kutoka kulia ni
Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Magila Tech iliyotengeneza Teknolojia ya Tigo Backup, Godfrey Magila na Ofisa Mtendaji Mkuu wa DTBi, Mhandisi George Mulamula
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Magila Tech iliyotengeneza Teknolojia ya Tigo
Backup, Godfrey Magila (kulia), akitoa maelezo kwa Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Dk. Binilith Mahenge jinsi kituo hicho cha oparesheni kinavyofanya kazi.Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI ya Mawasiliano ya simu ya Tigo
kwa kushirikiana na Kituo cha Kukuza Vijana Wenye Mawazo ya Sayansi na
Teknolojia (DTBi), wamezindua huduma itakayowawezesha watumiaji wa simu
za kisasa (smartphone) kurejesha kumbukumbu na kupatikana kwa simu
iliyopotea au kuibiwa.
Akizungumza kabla ya kuzinduliwa rasmi
huduma hiyo Makao Makuu ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia
(Costech), Dar es Salaam leo asubuhi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais Mazingira, Dk.Binilith Mahenge, Meneja Mkuu wa Tigo, Diego
Gutierrez, alisema huduma hiyo inaitwa 'Tigo Backup' itakuwa na uwezo wa
kurudisha majina yote kwenye simu, picha, video, ujumbe mfupi 'sms' na
vitu vingine vilivyopotea.
Alisema mteja ataweza kugundua na
kurejesha simu zao zilizopotea au kuibiwa na pia huduma hiyo
itamuwezesha mteja kuwa na uwezo wa kupata picha ya aliyemuibia kwani
simu itapiga king'ora.
" King'ora hicho kitaonesha simu ilipo,
simu itajifunga ili kuzuia matumizi mabaya, kumjulisha mwenye simu
pindi abadilishapo laini na kwamba huduma hiyo imebuniwa na mwanafunzi
mzawa kutoka DTBi ," alisema Gutierrez.
Kwa upande wa Waziri, Dk. Mahenge
alizishukuru kampuni hizo kuwajengea uwezo na kuwawezesha Watanzania
kuleta maendelea katika nchi yao na kujijengea utajiri kupitia ubunifu
huo.
Alisema Tanzania nchi inayoungwanishwa
kidigitali zaidi kwa kutumia sismu kuliko kompyuta na kwa mujibu wa
takwimu za watumiaji wa simu zinaonesha kuna ongezeko kubwa kutoka watu
milioni 2.96 mwaka 2005 hadi milioni 33 mwaka huu.
Alisema kwa kutambua nchi ni changa
ambayo watu wake asilimia 50 ni vijana, wamejikita katika kutoa elimu ya
ufundi katika sayansi na teknolojia yenye ubunifu.


0 comments:
Post a Comment