
Mgombea urais wa UKAWA Mh Edward Lowassa amesema akichaguliwa kuwa rais
wa awamu ya tano ataunda serikali itakayokuwa na viongozi wenye uwezo wa
kuchukua hatua na kutatua matatizo ya wananchi na atahakikisha
utaratibu wa wananchi kulalamika na viongozi pia kulalamika kama ilivyo
sasa unabaki kuwa historia.

Mh Lowassa ambaye amefanya mikutano minne katika majimbo ya Mtera, Bahi
Chilonwa na Dodoma mjini pia amewaomba watanzania kumpa nafasi ya
kukamilisha ndoto yake ya kuleta usawa wa huduma za kijamii ikiwemo
elimu aliyoanza kuonyesha mfano kupitia shule za kata alipokuwa waziri
mkuu.
Mheshimiwa Lowassa akizungumza

Awali waziri mkuu mstaafu wa awamu ya tatu Mh Fredrick Sumaye na
mwanasheria wa Chadema Mh Tundu Lisu wamesema kukithiri kwa malalamiko
ya wananchi kukosa huduma huku wanaotakiwa kuchukua hatua wakiendelea
kutoa ahadi inatosha kuonyesha kuwa uwezo wao wa kupata ufumbuzi umefika
mwisho na ndio maana UKAWA inaomba nafasi ya kuondoa tatizo hilo.
Wananchi na viongozi wa jimbo la Mtera wamesema ubinafsi wa viongozi wa
CCM, na ahadi zisizotekelezeka umesababisha wapoteze matumaini ya
kuondokana na umaskini hasa kwa vijana suala ambalo aliyekuwa naibu
waziri wa kazi na ajira Dr Makongoro Mahanga ambaye sasa amehamia UKAWA
alipata fursa ya kulitolea ufafanuzi.
Lowasa katika viwanja vya BARAFU Dodoma leo ameweka Historia katika
mkutano huo kwa umati mkubwa wa watu uliojitokeza kumlaki na
kumsikiliza.
Baada ya mkutano kumalizika wananchi hawakuridhika wakaamua kumsindikiza
hadi nyumbani kwake Dodoma na umati mkubwa sana uliwasili nyumbani
kwake wakifwatana na msafara wake jambo ambalo halikuwahi kutokea kwa
mgombea mwingine katika mji huo ambao ni mji mkuu wa Tanzania
Akihitimisha mikutano yake ya kampeni katika mkoa wa Dodoma uliofanyika
Dodoma mjini Mh Lowaasa ambaye sasa anaelekea mkoa wa Singida ameendelea
kunadi sera za UKAWA na kutoa ufafanuzi wa namna ya kuzitekeleza kwa
wakati na kwakasi inayostahili.

BOFYA HAPA CHINI UONE MAFURIKO YA HATARI YA MGOMBEA










0 comments:
Post a Comment