MWANASOKA
bora wa dunia, Cristiano Ronaldo amefunga mabao matano peke yake, Real
Madird ikiibuka na ushindi wa 6-0 ugenini dhidi ya Espanyol katika La
Liga usiku huu Uwanja wa Cornella-El Prat.
Mreno
huyo alifunga mabao yake katika dakika za saba, 17 kwa penalti, 20, 61
na 80 wakati bao lingine la Real likifungwa na Karim Benzema dakika ya
28.
Ronaldo
sasa anafikisha jumla ya mabao 230 katika mechi 204 za La Liga
alizocheza tangu ametua Real, akivunja rekodi ya gwiji wa zamani wa
klabu hiyo, Raul aliyefunga mabao 228 katika mechi 550.
Kikosi
cha Espanyol kilikuwa; Lopez, Arbilla, Alvaro, Ciani/Paco Montanes
dk46, Duarte, Victor/Joan Jordan dk64, Javi Lopez/Canas dk46, Alvarez,
Salva, Gerard na Caicedo.
Real
Madrid; Navas, Carvajal, Pepe, Ramos/Varane dk74, Marcelo, Casemiro,
Modric/Kovacic dk55, Isco, Bale, Ronaldo na Benzema/Vazquez dk62.
Ronaldo
akishangilia baada ya kuweka rekodi mpya ya mabao La Liga, kufuatia
kufunga mabao matano peke yake Uwanja wa Cornella-El Prat PICHA ZAIDI GONGA HAPA



0 comments:
Post a Comment