Mambo yakaendelea vizuri, ujenzi unasogea tu kwenye hatua ya kukamilika.
Juu ya mjengo kuna panel za Solar kwa sababu umeme unaotumika kwenye nyumba ni umeme wa nguvu ya jua (Solar Power).
Kilichotumika
kwenye ujenzi wote ni mabomba ya chuma na upande wa ukuta ni kioo
kitupu ukiwa ndani unaona kila kitu kinachoendelea nje.
Kwanza kabisa hii nyumba kila kitu kimeunganishwa na system ya App
ambayo mwenye nyumba yuko nayo kwenye simu yake, unaambiwa hata kama
vinywaji vimepungua kwenye fridge hana haja ya kufunua kuangalia, App ya
kwenye simu yake inampa majibu yote.
Hii
ndio App yenyewe mtu wangu, kama kuna mlango uko wazi, nini hakipo
kwenye friji, kuwasha na kuzima taa, vyote unavijua kupitia kwenye simu
yako.


0 comments:
Post a Comment