Sheikh
wa Mkoa wa Dar es Salaam, ambaye ni nahodha wa timu ya viongozi wa
dini, Alhadi Mussa Salum, akinyanyua juu kikombe cha ushindi wa pili
baada ya kumalizika kwa pambano la soka kati ya viongozi hao na mabalozi
kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam leo Oktoba 17, 2015.
Mabalozi walishinda kwa mikwaju ya penati 3-2 na kutwaa kombe. Katikati
ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, na wakwanza ushoto
ni Meneja Mkuu wa kampuni ya Acacia, anayeshughulikia ustawi wa kampuni, Assa Mwaipopo
NA K-VIS MEDIA
KAMPUNI
ya Acacia imedhamini pambano la soka kati ya viongozi wa dini na
mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa Tanzania, pambano lililopigwa
uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana Oktoba 17, 2015
Katika pambano hilo, mabalozi waliibuka washindi kwa njia ya mikwaju ya penalty 3-2 na kutwaa kombe.
Akitoa
nasaha zake kabla ya kuanza pambano hilo la kuenzi amani taifa
linapoelekea kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwezi
huu, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, aliwaambia
washiriki kuwa, serikali inaunga mkono jitihada za viongozi wa dini na
mabalozi katika kuwaleta pamoja wananchi hususan katika kipindi hiki
ambacho taifa linaelekea kwenye uchaguzi.
Pambano
hilo la soka lililodumu kwa muda wa dakika 40, lilikuwa la utangulizi
kabla ya pambano la ligi kuu soka Tanzania bara kati ya Yanga na Azam
FC.
Akizungumza mwishoni mwa mchezo huo, Meneja Mkuu wa Acacia anayeshugulikia a ustawi wa kampuni, Assa
Mwaipopo, alisema, kampuni yake imedhamini pambano hilo kwa kutambua
umuhimu wa amani hapa nchini, ambapo Acacia kama wawekezaji wanao wajibu
wa kuunga mkono jitihada zozote za kijamii katika kuhakikisha amani
inakuwepo hapa nchini inakuwepo.
“Sote
tunatambua kuwa hivi karibuni taifa litaingiankwenye uchaguzi mkuu wa
kuchagua viongozi wetu, hivyo pambano hili la soka la viongozi wa dini
na mabalozi ambalo nia yake kubwa ni kuhamasisha amani miongoni mwa
Watanzania katika kipindi hiki cha uchaguzi limekuja wakati muafaka nasi
kama Acacia tumeona tuchangie katika jambo hili muhimui.” Alisema Assa.
Katika
pambano hilo lililofana, wachezaji wa timu zote mbili walionyesha
ukakamavu wa hali ya juu kwa kumudu kucheza kwa nguvu na umahiri mkubwa
na kuwapa burudani safi wapenzi wa soka.
Balozi wa Jumuiya ya Ulaya hapa nchini, Filiberto
Sebregondi, ambaye alikuwa nahodha wa timu ya soka ya mabalozi,
akinyanyua juu kombe baada ya timu yake kuishinda timu ya mabalozi
kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2015.
Wanaoshuhudia kushoto ni Meneja Mkuu wa kampuni ya Acacia,
anayeshughulikia ustawi wa kampuni, Assa Mwaipopo, na Mkuu wa Mahusiano
ya Serikali, Alex Lugendo (wapili kushoto)
Waziri Chikawe, (kushoto), akisalimiana na Assa Mwaipopo
Chikawe, akisalimiana na Alex Lugendo
"Ball Boys" wakiwa wamebeba bendera ya Acacia, wakati timu zikiingia uwanjani
Sheikh Alhadi akiwa kwenye mazoezi ya viungo na viongozi wenzake wa dini kabla ya mpambano huo
Sheikh Alhadi akifumua shuti
Mwamuzi wa pambano hilo Kamishna wa Polisi na Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, akipuliza kipyenga
Sheikh Alhadi akijaribu kufunga penalty ambayo hata hivyo hakufanuikiwa kufunga
Timu ya viongozi wa dini iliyomenyana na mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini
Timu ya soka ya mabalozi na wakuu wa mashirika ya kimataifa wanaowakilisha mashiorika na nchi zao hapa nchini
Waziri Chikawe, viongozi wa Acacia, na wale wa TFF wakisalimiana na wachezaji wa timu zote mbili
Viongozi wa dini wakiongozwa na kocha wao wakati "wakipasha" kabla ya pambano hilo
Meneja
Mkuu wa kampuni ya Acacia, anayeshughulikia ustawi wa kampuni, Assa
Mwaipopo, akiwaeleza waandishi wa habari sababu za kampuni hiyo
mudhamini pambano hilo la soka.“Sote
tunatambua kuwa hivi karibuni taifa litaingiankwenye uchaguzi mkuu wa
kuchagua viongozi wetu, hivyo pambano hili la soka la viongozi wa dini
na mabalozi ambalo nia yake kubwa ni kuhamasisha amani miongoni mwa
Watanzania katika kipindi hiki cha uchaguzi limekuja wakati muafaka nasi
kama Acacia tumeona tuchangie katika jambo hili muhimui.” Alisema Assa.
"Benchi
la ufundi" la viongozi wa dini, kutoka kushoto, Sheikh Basaleh, Mkuu wa
wilaya ya Temeke, Sophia Mjema, na Sheikh Othman, wakifuatilia kwa
karibu pambano hilo
Nasaha za mgeni rasmi kwa timu zote mbili
Waziri
Chikawe, (kulia), akiongozana na Assa Mwaipopo, (kushoto) na Mkuu wa
Mahusiano ya Serikali wa kampuni ya Acacia, Alex Lugendo, mara baada ya
ukaguzi wa timu
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, (kushoto), ambaye alikuwa kamisaa wa mchezo aisalimiana na Assa Mwaipopo
Mazoezi ya viungo yakiendelea
0 comments:
Post a Comment