https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    BAADA YA KIPIGO CHA TATU HUU NDIO UCHAMBUZI WA MDAU CHIKOTI





    Chelsea 1-3 Southampton
    1. Jose Mourinho sijui kama anajielewa na kama anaeleweka na kama anaielewa timu yake tena kwasasa, ni kama vile kila mchezaji anacheza anavyotaka na sio inavyotakiwa.
    2. Chelsea ukiachana na Begovic hakuna eneo lililo bora ama salama tena, viungo wako hovyo, washambuliaji ni shida na mabeki ndiyo majanga kabisa, kiujumla unaweza sema ni timu nzuri kwenye makaratasi na labda PS pia.
    3. Matic ameingia kipindi cha pili na kutolewa baada ya dk 28 tu bila hata ya kupewa mkono na Jose, labda tutaambiwa ni mbinu lakini mmmmh mpaka mashabiki baadhi walizomea hapa kuna kitu zaidi, nyuma ya pazia ni kama vita ya ndani.
    4. Kwasasa kuna Chelsea, Jose Mourinho na kuna wachezaji yaani hapa kuna makundi matatu ambayo hayaelewani, hii unaweza kusema wote wanajenga nyumba moja lakini wanagombania nguzo.
    5. Narejea tena maneno haya, Roman Abramavich ni BOSI na Jose Mourinho ni MFANYAKAZI WAKE. Hii ni sentensi ndogo lakini ina uzito wake pale ambapo Mrusi ataamua kuwa Mrusi kweli.
    6. Hata sielewi kwanini Depay yuko Manchester United na Sado Mane yuko Soton?
    NB: ‪#‎JOSEOUT‬. haya maneno naona kama soon yatapata watamkaji.
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: BAADA YA KIPIGO CHA TATU HUU NDIO UCHAMBUZI WA MDAU CHIKOTI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top