Mechi ya mwisho kwenye La Liga Barcelona ilichezea kichapo kutoka kwa Sevilla ambapo matokeo yalikua Sevilla 2 Barcelona 1. Baada ya kupoteza mechi ile maneno mengi yalisemwa kwamba Barcelona bila Messi hakuna kitu.
Sasa leo hii wanaingia uwanjani kwenye ku-prove wrong hayo maneno. Kikosi kikiwa na mastaa kama Neymar na Suarez wanategemewa kuongoza timu kuchukua point 3 muhimu kwenye mechi dhidi ya Rayo Vallecano.
Rayo ipo nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi, La Liga ni ligi ambayo hauwezi kusema club kubwa lazima itaifunga club ndogo. Hata club ya chini inaweza kuifunga club ambayo inaongoza ligi. Macho na maskio ya watu wengi wanataka sana kuona bingwa mtetezi wa Ulaya na Hispania inavunja mwiko wa kutokushinda bila kuwa na Messi kwenye La Liga.
Mechi ni saa 9:30 Jumamosi October 17 kupitia AzamSportsHD ikiwa ni moja ya mfululizo wa mcechi za Soka Fiesta. Sit back relax nyumbani au sehemu yoyote Azam TV wameshafanikisha La Liga kwa bei nafuu.
0 comments:
Post a Comment