BREAKING NEWS : WATU 6 WAFARIKI KATIKA AJALI YA BARABARANI MOROGORO
Watu
sita wamefariki dunia baada ya gari ndogo waliokuwa wakisafiria
kugongana uso kwa uso na basi la abiria mali ya kampuni ya Princess
Muro, lililokuwa likitokea Dar es salaam kuelekea Tunduma, katika eneo
la hifadhi ya taifa ya Mikumi, barabara kuu ya Morogoro-Iringa. Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Morogoro Leonard Paulo amethibitisha kutokea kwa
ajali hiyo katika eneo la hifadhi ya taifa ya Mikumi, ikihusisha gari
ndogo la abiria aina ya Toyota Noah lenye namba za usajili T 359 BBA
iliyokuwa imebeba abiria sita wakiwemo wanawake wawili na wanaume wanne
ambayo ilipasuka tairi ya Mbele ya kuyumba ovyo barabarani na kugongana
na basi hilo la Princess Muro lenye namba T 160 BBC na kusababisha vifo
kwa abiria wote wa Noah.
0 comments:
Post a Comment