Mtandao wa
asasi za kiraia wa kuangalia uchaguzi nchini Tanzania TACCEO umelaani vikali
kitendo cha jeshi la polisi kuvamia kituo cha ukusanyaji wa matukio mbalimbali
yaliyokuwa yanajili wakati mchakato wa uchaguzi ulipokuwa unaendelea na
kuchukua baadhi ya vifaa vya kituo hicho na kuwakamata baadhi ya maafisa wake.
Akizungumza
na waandishi wa habari mapema leo KAIMU MWENYEKITI WA UMOJA HUO BW HEBLON
MWAKAGENDA amesema kuwa tukio hilo lilitokea octoba 29 majira ya saa nane
katika eneo la mbezi bichi eneo ambalo kituo hicho kilikuwepo.
Bwana
Mwakagenda amebainisha kuwa wakiwa kazini walishuhudia gari ya jeshi ya polisi
ambayo ilikuwa na polisi sita waliokuwa wamevaa mavazi ya kujihami pamoja na
silaha za moto wakiingia kituoni hapo ambapo askari hao walianza kuchukua vifaa
vyao mbalimbali walivyokuwa wanafanyia kazi zikiwemo kompyuta za mezani
25,kompyuta mpakato 3 simu 25 za ofisini na kuwakamata waanglizi wao 36.
Aidha
Bwana Mwakagenda ameeleza kuwa matukio ambayo yanafanywa na jeshi la polisi
yanatakiwa kulaaniwa na kila mpenda Demokrasia maana yanalenga katika
kudhoofisha demokrasia nchini ambayo ndo msingi wa utawala bora
Hata hivyo
BW MWAKAGENDA ameitaka selikali kutotumia vyombo vya dola katika
michakato yeyote ya kidemokrasia kwani kwa kufanya hivo kunaweza kuleta
uvunjifu wa amani iliyojengwa kwa mda mrefu.
Kaimu mkutugenzi wa LHRC ambao ni wataribu wa mtandao huo IMELDA LULU URIO akizungumza katika mkutano huo |
Ameongeza
kuwa swala hilo limetokea huku vyombo vya dola vikitambua wazi kuwa uangalizi
huo wa uchaguzi ulifwata misingi yote iliyowekwa kikatiba na sheria pamoja na
kuwa na vibali na vitambulisho maalum kutoka tume ya uchaguzi vilivyowaruhusu
kufanya kazi hiyo kihalali.
Akizngumza na wanahabari katika mkutano huo Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na haki za binadamu nchini Tanzania LHRC ambao ndio waratibu wa mtandao huo Bi IMELDA LULU URIO amesema kuwa tukio la kuvamiwa kwa waangalizi wao na jeshi la polisi sio la kwanza kwani wakati waangalizi hao wakifwatilia zoezi la uandikishwaji wa daftari la kudumu la mpiga kura kwa mfumo wa BVR huko Njombe waangalizi wao walivamiwa na polisi na kupigwa wakiwa katika kazi zao na hadi leo hakuna ufafanuzi wowote uliotolewa na mamlaka husika kuhusu chanzo cha tukio hilo.
0 comments:
Post a Comment