Ishara za mapema kutoka kwa
kura ya maoni kuhusu uhalalishaji wa ndoa za jinsia moja nchini Ireland
zinaonyesha kuwa wanaounga mkono ndoa hizo wanaelekea kupata ushindi
mkubwa.
Kura zinaendelea kuhesabiwa na matokeo rasmi yanatarijiwa kutangazwa baadaye leo.
Lakini mawaziri wa serikali
ambao wanaunga mkono mabadiliko hayo ya kikatiba,wameielezea siku ya
leo kama ya kihistoria huku wengi waliopinga kura hiyo wakiwapongeza
waliounga mkono sheria hiyo ya ndoa za jinsia moja.
Iwapo mabadiliko hayo yataidhinishwa,Ireland itakuwa nchi ya kwanza kuruhusu ndoa za jinsia moja kupitia wingi wa kura



Hakika ni anguko la maadili.
ReplyDelete