Katika taarifa yake fupi kwa umma ambayo Swahilivilla imepata nakala yake,
ZADIA ilimnukulu Bwana
Othman akisema kuwa Katiba ya Zanzibar inampa
kila Mzanzibari wajibu wa kulinda, kuhifadhi na kudumisha Uhuru wa
Zanzibar, Mamlaka ya Zanzibar, Ardhi ya Zanzibar na Umoja wa
Zanzibar.
"Maelezo
hayo ya Mheshimwia Othman, yanakwenda sambamba na malengo makuu ya
Jumuiya ya Wazanzibari waishio nchini Marekani (ZADIA)", ilisema taarifa
hiyo, na kusisitiza "Kwa hivyo, ZADIA inapenda kuchukua fursa hii
kumpongeza na kumuunga mkono Mheshimiwa Othman Massoud Othman kwa kauli
zake hizo za kizalendo.
Taarifa
ya ZADIA iliyosainiwa na mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Bwana Omar Haji
Ali, imeendelea kuelezea juu ya Bwana Othman alivyowakumbusha
Wazanzibari jinsi alivyotekeleza wajibu wake huo wa kikatiba kivitendo
kwa kupiga kura "kama alivyopiga" kwenye Bunge Maalum la Katiba mjini
Dodoma.
Aidha
taarifa hiyo imemkariri msomi huyo wa Sheria akizifafanua kasoro
zilizomo kwenye Katiba pendekezwa ya Tanzania ambayo aliielezea kuwa
haina maslahi kwa Zanzibar.
"Kitendo
hicho cha kijasiri, na maelezo hayo, vinatoa changamoto kwa Kila
Mzanzibari kuiga mfano huo. Nasi Wanadiaspora tumezipokea kwa moyo wote
changamoto hizo na kuzifanyia kazi kama ambavyo imekuwa kawaida yetu. Na
tutafanya juhudi zote na tutashirikiana na wadau wote, ili kuhakikisha
kuwa Zanzibar inapata hadhi yake na haki zake ndani ya Muungano wa
Tanzania", imemalizia taarifa ya ZADIA.
Itakumbukwa
kuwa Mheshimiwa Othman Massoud Othman, alikuwa ni miongoni mwa
Wazanzibari waliopiga kura za wazi za "hapana" kwenye Bunge Maalum La
Katiba mjini Dodoma kupinga rasimu ya Katiba mpya ya Jamhuri a Muungano
wa Tanzania kwa vile ilikuwa inaikandamiza Zanzibar.
Kitendo
hicho kilizingatiwa na Wazanzibari wengi kuwa ni cha kijasiri na
kizalendo, lakini wachambuzi wanaona kuwa ilikuwa ndiyo sababu ya
kuvuliwa wadhifa wake kama Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar.
0 comments:
Post a Comment