ORODHA YA WACHEZA SOKA 10 WENYE MVUTO ZAIDI DUNIANI
Mtandao wa www.sokkaa.com umetoa orodha ya wanasoka 10 wenye mvuto aidi duniani ‘Most Handsome Footballers in the World’.
Hii hapa ni orodha kamili;
10. Mats Hummels-Borussi Drtmund
Mats
Hummels ni mchezaji wa kijerumani anaekipiga kwenye klabu ya Dortimnd
ambaye kwa sasa ni nahodha wa kikosi hicho. Ana mwonekano ambao wanawake
wanaoshabikia mchezo wa mpira wa miguu wamekuwa wamekuwa na maswali
mengi juu ya mwanandinga huyo.
9. Gerrard Piqué–FC Barcelona
Macho
yake ya blue na style ya nywele zake, Gerrard Pique anakamata nafasi ya
tisa kwenye orodha ya wachezaji wa mpira wenye mvuto zaidi.
8. Cesc Fabregas-Chelsea
Ni
miongoni mwa viungo wachezeshaji kwenye ligi ya England (EPL) Mbali na
uwezo wake wa kupiga pasi, Fabregas pia ni mwanaume mwenye mvuto na
anashika namba nane kwenye orodha hii.
7. Mario Gotze-Bayern Munich
Ni
kiungo wa klabu ya Bayern Munich ambaye alipata heshima kubwa nchini
Ujerumani kwenye historia ya soka baada ya kufunga goli la ushindi kwa
Ujerumani mwaka 2014 dhidi ya Argentina.
6. Fernando Torres-Atletico Madrid
Fernando
Tores a.k.a ‘El Nino’ amewatesa watoto wengi wa kike wanashabikia mpira
kutokana na mvuto wa sura yake, stayle ya nywele na umbo la mwili wake
ambalo limebalansiwa vizuri.
5. Van Persie-Fenerbahce S.K.
Robin
van Persie siku za hivi karibuni amepachikwa jina la utani ‘The Flying
Dutchman’ kutokana na goli alilofunga kwa kichwa wakati Uholanzi
inacheza dhidi ya Hispania kwenye michuano ya kombe la dunia mwaka 2014.
4. Iker Casillas–Real Madrid
Iker Casillas bado ni miongoni mwa magolikipa bora ulimwenguni na ni miongoni mwa wacheza mpira wenye mvuto zaidi duniani.
3. David Villa–New York City FC
Mbali na kufunga magoli mazuri, Villa amengia kwenye orodha ya wachezaji wenye mvuto pamoja na style nzuri ya nwele zake.
2. Kaka–Orlando City FC
Ricardo
Kaka anashika nafasi ya pili kwenye orodha hii. Muonekano wake wa
kuvutia pamoja na style ya nywele, vilifungua milango ya yeye kuingia
kwenye tasnia ya fashion. kampuni nyingi za fashion zimekuwa zikimsaka
mkali huyo kwa ajili ya kufanya nae matangazo.
1. Cristiano Ronaldo-Real Madrid
Nyota
huyo wa Real Madrid ni mchezaji wa mpira wa miguu mwenye mvuto zaidi
duniani. Ni miongoni mwa wacheza mpira wachache ambao wanawafanya
mashabiki wengi wa soka kuangalia mchezo huo. Mvuto wa sura, style ya
nywele na umbo zuri ni baadhi ya vitu vinavyowachanganya watoto wa kike.
0 comments:
Post a Comment