Dharura inaweza kutokea popote na wakati
wowote, unaweza kupata picha hofu utakayokuwa nayo ikitokea mko
katikati ya safari kwenye Ndege angani alafu Rubani anafariki !!
Ndege ya American Airlines iliyokuwa imetoka Phoenix kwenda Boston Marekani imelazimika kutua kwa dharura Uwanja wa Syracuse, Hancock International Airport New York baada ya Rubani wa Ndege hiyo, Michael Johnston kufariki…
Kifo chake ilikuwa ghafla tu ambapo baada ya hali yake kuwa mbaya
alianza kupata huduma ya msaada kutoka kwa mmoja ya wahudumu wa Ndege
lakini muda mfupi baadae akafariki.
Msemaji wa Shirika la Ndege la American Airlines amesema
Ndege ilitua salama kwa sababu ndani alikuwemo pia Rubani msaidizi, na
kilichosaidia pia ni Sheria inayolazimisha kila ndege kuwa na Marubani
wawili ndani.
Ndege ilikuwa na jumla ya Abiria 147, mpaka sasa sababu ya kifo chake haijafahamika japo mkewe anasema huenda Michael Johnston alifariki kwa tatizo la pressure.
Taarifa ya stori yenyewe iko pia kwenye kipande hiki cha Video.
0 comments:
Post a Comment