https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    UVAAJI WA VIATU VIREFU UNAWEZA KUKUSABABISHIA MADHARA YA KIAFYA. SOMA HAPA!

    Wanawake wengi kwa kawaida hupenda kuonekana warembo na wenye kupendeza muda wote yaani kuanzia mavazi, vipodozi vya mwilini hadi viatu pia.

    Wakinadada wengi katika harakati zao za kuhitaji kuonekana warembo zaidi hupenda pia kuvaa viatu vizuri na baadhi ya hupendelea viwe virefu.

    Viatu virefu ‘mchuchumio’ au viatu vyenye visigino virefu ni miongoni mwa viatu vinavyopendwa na wasichana wengi hapa nchini na hata nje pia, lakini wataalam kusababisha madhara kwa mhusika pia.

    Wataalam wanaeleza kuwa viatu hivyo huweza kusababisha uharibifu wa pingili za uti wa mgongo sambamba na kuvunjavunja mifupa ya visigino.

    Kwa kawaida viatu hivi virefu hupendwa zaidi na wasichana wafupi wakiwa na lengo la kuonekana warefu kidogo angalau.
    Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali zinaonesha kuwa viatu virefu havifai hata kidogo. Kutokana na viatu hivyo kusababisha maumivu makali ya misuli ya miguu pamoja na nyama za nyuma kwenye maungio ya magoti na enka.

    Mbali na madhara hayo pia huweza kuchangia uharibifu wa ndani ya magoti kwa kuhamisha maungio. Kulingana na namna mhusika jinsi anapovaa viatu virefu kwa muda mrefu, ndipo inaposababisha madhara ya muda mrefu pia.

    Aidha viatu virefu pia  huchangia kusababisha mwili kukosa usawa wakati wa kutembea, kupoteza mwelekeo na mwendo halisi na misuli ya miguu kubana, huku wakati mwingine huweza kusababisha hata mhusika kuanguka.

    Pia viatu virefu husababisha maumivu makali ya kidole gumba cha mguu na hata kuchangia katika kuzuia ukuaji wa kucha pia.
    Inapendekezwa kuvaa viatu virefu kuwe kwa muda maalumu kwa shughuli maalumu na viatu husika visizidi urefu wa inchi mbili.

    Baada ya kuyafahamu hayo machache ni vyema sasa ukazingatia afya yako wewe mwanamke au msichana kwani kumbuka kuwa pamoja na kutaka urembo, lazima ujali afya yako jambo zuri zaidi ni kuangalia madhara kwa baadaye kuliko kukimbilia kuvaa viatu virefu kwa ajili ya urembo.
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: UVAAJI WA VIATU VIREFU UNAWEZA KUKUSABABISHIA MADHARA YA KIAFYA. SOMA HAPA! Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top