Serikali inapenda kukanusha taarifa kutoka Kwenye baadhi ya Mitandao
ya Kijamii ikidai kwamba, Mhe. Dkt. Abdallah Kigoda, Waziri wa Viwanda
na Biashara amefariki dunia nchini India alikokuwa anatibiwa.
Taarifa rasmi ya serikali ni kwamba taarifa hizo ni za uongo na hazina hata Chembe ya ukweli. Mhe. Dkt. Kigoda bado yupo nchini India Katika Hospitali ya Apollo katika Jiji la New Delhi anakoendelea kupatiwa matibabu.
Mhe. Dkt. Kigoda alikwenda India kwa matibabu tarehe 18 Septemba, 2015 na tangu kipindi hicho ameendeleaa kupata matibabu katika hospitali Hiyo ya Apollo.
Serikali inapenda kuvionya vyombo vya habari na Mitandao ya kijamii kuacha kusambaza taarifa za uongo kuhusu viongozi wa serikali.
Imetolewa na Assah Mwambene, Msemaji Mkuu wa Serikali.

0 comments:
Post a Comment