KLABU
ya Simba SC imelalamika kwamba, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)
haliwatendei haki kwa sababu uongozi wake umesheheni watu wa Yanga SC.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe ameiambia BIN
ZUBEIRY SPORTS- ONLINE leo kwamba, imefikia TFF wamekata kabisa
mawasiliano na klabu yao.
Poppe amesema kwamba TFF sasa hawajibu hata barua za Simba SC wanapoandika kuhoji au kuomba ufafanuzi wa jambo lolote.
Kapteni
huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) amesema kwamba
imefikia wakati wanashindwa hata kujua namna gani wanaweza kupata haki
zao nyingine za msingi, kutokana na ‘kuchuniwa’ na TFF.
“Inafahamika
kwamba Rais wa TFF (Jamal Malinzi), Katibu wake (Mwesigwa Selestine)
wote ni Makatibu wa zamani wa mahasimu wetu, Yanga SC. Na bado wapo
wengine wengi pale TFF ambao wametoka Yanga akina Baraka Kizuguto.
“Lakini
kwa sababu wanaongoza chombo cha kitaifa, wanapaswa kutenda haki, yaani
inaonekana kabisa TFF wanaikandamiza Simba na wanaibebea
Yanga,”amelalamika Poppe.
Akifafanua,
mfanyabiashara huyo maarufu nchini, amesema TFF hawajajibu barua yoyote
ya Simba SC kwa mwaka huu na hawaelewei sababu ni nini.
“Watuonyeshe
wao, ni barya ipi ya Simba SC wamejibu mwaka huu, malalamiko yetu ya
mchezo dhidi Yanga hawakujibu, Suala la Messi (Ramadhani Singano)
hawakujibu. Hata tunapojibu barua zao za adhabu wanazotuandika ili
kuomba ufafanuzi, pia hawatujibu.
“Labda
watuambie basi kwamba barua zetu tunatakiwa kuzipitishia Yanga SC ndiyo
watujibu, tutafanya hivyo, tutaandika na kuwapelekea Yanga waweke
muhuri wao ipelekwe TFF, tujibiwe, hiyo ndiyo shida yetu,”amesema.
Hans
Poppe amesema kwamba mchezaji wao Ramadhani Singano ‘Messi’
amehamishiwa Azam FC kinyume cha utaratibu na kila wapodai haki yao
hawasikilizwi. “Mchezaji wa Yanga (Donald Ngoma) alimpiga kichwa
mchezaji wetu (Hassan Kessy) na tukapeleka ushahidi wa picha za video,
hakuchukuliwa hatua na wala hatukujibiwa,”.
“Lakini
Juma Nyosso (wa Mbeya City) alimdhalilisha John Bocco (wa Azam FC)
akachukuliwa hatua baada ya saa 24 kwa ushahidi wa picha,”amesema.
Aidha,
amesema kwamba Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), limeiamuru klabu
ya Etoile du Sahel ya Tunisia iilipe Simba SC dola 300,000 za
Kimarekani za manunuzi ya mshmbauliaji Emmanuel Okwi, lakini wanashindwa
kufuatulia kwa sababu TFF haiwasikilizi tena.
“Kwa
kweli tupo wakati mgumu mno, tunashindwa hata kuelewa tunacheza hii
ligi kwa sababu gani, inaonekana tunawasindikiza watu ambao tayairi
wameandaliwa kwa namna yoyote wawe mabingwa,”amesema
Hans Poppe amesema TFF haiwatendeo haki kwa sababu viongozi wengi ni Yanga SC |
0 comments:
Post a Comment