Nchi za wanachama wa Umoja wa Ulaya
zimeridhia mpango wa utekelezaji kwa Uturuki, ambao unatarajiwa
kusadia kupunguza wimbi la wahamiaji wanaoingia Ulaya.
Karibu wahamiaji laki 6 wameingia
katika nchi za Umoja wa Ulaya mwaka huu, wengi wao wakitokea Uturuki
na kuingia Ugiriki wakijaribu kwenda kaskazini.
Uturuki imetoa masharti ya mambo
inayohitaji ili iweze kusaidia kudhibiti kuingia kwa wakimbizi nchi
za Umoja wa Ulaya.
Akiongea na vyombo vya habari Jijini
Brussels, rais wa Baraza la Ulaya, Bw. Donald Tusk, amesema anahisi
matumaini kutokana na makubaliano hayo.
0 comments:
Post a Comment