Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
inapenda kutoa taarifa kwa umma kuhusu utangazaji wa matokeo ya Uchaguzi Mkuu
kwa vyombo vya utangazaji kwa mujibu wa Kanuni za Huduma za Utangazaji (Maudhui)
(Utangazaji wa Uchaguzi wa Vyama vya Siasa), 2015. Kanuni hizi zipo kwa mujibu
wa Sheria kama ilivyotolewa na Gazeti la Serikali la Tarehe 26 Juni, 2015.
Kanuni hizi zinalenga kuweka utaratibu mzuri wa kutangaza shughuli za kampeni
na uchaguzi mkuu kuwa wa amani na utulivu.
Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania inapenda kuwakumbusha kuwa ni marufuku kwa vituo vyote
vya utangazaji kutangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu bila kupata taarifa sahihi
kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa utaratibu waliojiwekea.
Vilevile,
vituo vyote vya utangazaji vinapaswa kuzigatia Sheria na Kanuni za Huduma za
Utangazaji (Maudhui) (Utangazaji wa Uchaguzi wa Vyama vya Siasa), 2015.
Kanuni
za Huduma za Utangazaji (Maudhui) (Utangazaji wa Uchaguzi wa Vyama vya Siasa),
2015, Na. 16 (1) na 16(2) inaelekeza kama ifuatavyo:-
16(1) kwamba kila mtoa huduma za maudhui atakuwa na wajibu wa kuuarifu umma juu ya
matokeo ya uchaguzi, kadiri yanavyopatikana.
uangalizi maalumu ufanyike kuhakikisha
usahihi wa matokeo yote
yanayotangazwa.
16(2) Mtoa huduma za maudhui hatatangaza maoni ambayo
yanaweza kuchochea vurugu au kuhamasisha chuki kwa misingi ya mbari, kabila, jinsia,
dini au Imani za kisiasa na ambayo
yanajenga uchochezi wa kusababisha madhara.
Hivyo basi, vituo vya
utangazaji vinatakiwa kufuata kikamilifu Kanuni za Huduma za Utangazaji (Maudhui)
(Utangazaji wa Uchaguzi wa Vyama vya Siasa), 2015 na kwamba vituo vya
utangazaji vitawajibika na matokeo ya maudhui ya matangazo ambayo
hayatozingatia Kanuni.
Mamlaka inatoa wito kwa vituo vya utangazaji
kutumia weledi katika maamuzi ya kihariri kuchanganua kipi kinafaa kutangazwa na
uangalizi maalumu ufanyike kuhakikisha kuna
usahihi katika kutangaza matokeo yote yatakayotolewa na Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC).
IMETOLEWA
NA:
MKURUGENZI
MKUU
MAMLAKA
YA MAWASILIANO TANZANIA
TAREHE
25/10/2015
0 comments:
Post a Comment