Dorine akiwa hospitali baada ya kuchomwa mikono na shangazi yake.
Niukatili
ulioje ambao amefanyiwa mtoto Dorine (12), denti wa darasa la nne Shule
ya Msingi Makabe, Mbezi jijini Dar.Dorine anadaiwa kuunguzwa na maji ya
moto yaliyochemshwa kwenye jiko la gesi na walezi wake wa karibu
akiwemo shangazi yake aliyetajwa kwa jina moja la Scola ambaye alitiwa
mbaroni na bibi yake ambaye haikujikana alipo.Katika tukio hilo la
Septemba 26, mwaka huu, Scola alidaiwa kutekeleza tendo hilo, chanzo
kikielezwa ni upotevu wa shilingi 20,000.Kwa mujibu wa chanzo makini,
Scola alimtaka Dorine aseme amezipeleka wapi fedha hizo, lakini binti
huyo alisema hajui chochote.
Ilidaiwa
kwamba, katika hali isiyokuwa ya kibinadamu, wakati Dorine akiwa
anahojiwa tayari maji ya moto yalikuwa yakichemka.Ilisemekana kwamba,
baada ya kuona Dorine hataki kusema zilipo fedha hizo, Scola akamuamuru
aingize mikono ndani ya sufuria lililokuwa jikoni huku maji yakichemka.
Dorine
alipokataa, Scola akadaiwa kumshika kwa nguvu, akisaidiana na mama yake
ambaye ni bibi wa Dorine na kuizamisha kwenye sufuria la maji mikono
hiyo na kumsababishia mtoto huyo majeraha ya kutisha.
Ilisemekana
kwamba, baada ya tukio hilo, familia hiyo ilifanya siri kubwa na
kutompeleka hospitalini lakini baadhi ya majirani walibaini hilo na
kusambaza taarifa ndipo familia hiyo ikampeleka hospitalini kwa siri.
....Akisaidiwa na nesi kuinuka.
Alipofikishwa
katika Hospitali ya Kanisa Katoliki Luguruni, Mbezi mtoto huyo alilazwa
baada ya mahojiano na wauguzi ambapo aliwaeleza kila kilichotokea.Hata
hivyo, maelezo ya Dorine kwamba aliunguzwa na shangazi na bibi yake
yalipingwa na Scola ambaye alisema mtoto huyo alikuwa akikimbia
akaangukia maji ya moto.
Taarifa
alizopata mwanahabari wetu kwenye hospitali hiyo kupitia muuguzi wa
zamu, zilieleza kuwa taarifa sahihi za tukio hilo ni zile alizozitoa
mtoto huyo.Katika mahojiano na wauguzi, Dorine ambaye alikuwa amelazwa
kwenye Chumba cha Stuff Na. 16 hospitalini hapo, alifafanua kuwa anaishi
kwa shangazi yake baada ya baba yake mzazi kuachana na mama yake na
baba kuoa mwanamke mwingine.
Uchunguzi
uliofanywa na gazeti hili ulibaini kwamba, Scola alishikiliwa na Jeshi
Polisi Kituo cha Mbezi-Kwayusuf na baadaye aliachiwa kwa dhamana lakini
bibi hakukamatwa.
Kamanda
wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, RPC Camilius Wambura alipoulizwa na
gazeti hili juu ya tukio hilo alikiri kulijua na kwamba alipokea taarifa
za aina mbili hivyo alimwagiza OCD wa Mbezi-Kwayusuf kulifuatilia na
kumpa taarifa kamili.
Alisema
taarifa moja ilidai, Dorine aliunguzwa lakini ya pili ilidai aliangukia
kwenye sufuria yenye maji ya moto hivyo uchunguzi unaendelea ili kupata
taarifa kamili.


0 comments:
Post a Comment