Viongozi wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wamesema baada ya kufuatilia mwenendo wa Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wana taarifa za uhakika kwamba Maalim Seif Sharif Hamad, Mgombea Urais wa Chama cha Wananchi (Cuf) anayeungwa mkono na Umoja huo, ameshinda urais wa Zanzibar.
Taarifa iliyotolewa na viongozi hao jana kwa vyombo vya habari imetoa masharti manne kufuatia kufutwa kwa uchaguzi wa Zanzibar.
Sharti la kwanza ni kuzitaka mamlaka zinazosimamia Uchaguzi Mkuu huo kuondoa mara moja tangazo la kuufuta Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar.
Sharti la pili ni
kumtangaza Seif kuwa ni mshindi halali wa nafasi ya urais na hivyo
aapishwe kuwa Rais wa nchi ya Zanzibar ambayo ni sehemu ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
Sharti la tatu,
wametoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa kuingilia kati na kulaani kwa
nguvu zote kinachofanyika Zanzibar ambako kwa mara nyingine tena
demokrasia inataka kuminywa wazi wazi ili tu kuinusuru CCM isiondoke
madarakani kama ambavyo wapiga kura wamekuwa wakiamua.
Aidha sharti la nne ni kwa wananchi wa Zanzibar, “tunapenda kuwahakikishia kuwa tuko nao pamoja katika kipindi hiki kigumu cha kupigania mabadiliko .
Aidha sharti la nne ni kwa wananchi wa Zanzibar, “tunapenda kuwahakikishia kuwa tuko nao pamoja katika kipindi hiki kigumu cha kupigania mabadiliko .
Kura za Urais
Aidha
wamedai ushindi wa urais umetengenezwa, kwenye taarifa rasmi ya NEC
ambayo imetangaza hadharani na kunukuliwa kwenye vyombo vya habari
kwamba; wapiga kura walikuwa 15,589,639.
Katika
uchaguzi huo kura zilizopigwa 15,193,862 na kati ya hizo zilizoharibika
ni 402,248:”Kupitia hesabu hizo hapo juu unaweza kushuhudia upikwaji na
utengenezwaji wa matokeo uliofanywa ili kuhujumu matokeo ya Lowassa kwa
ajili ya kumbeba na kumpatia ushindi Dk. Magufuli ili kuinusuru CCM.”
Viongozi
hao walisema Ili kuthibitisha kauli yao kwamba wameongoza uchaguzi
katika nafasi hiyo kwa Lowassa ndiye Rais aliyechaguliwa na Watanzania
walio wengi walioshiriki uchaguzi Mkuu Oktoba 25.
“Tunazitaka
mamlaka zinazohusika, kwa mujibu wa katiba, sheria na taratibu za
uchaguzi, zitengue matokeo batili waliyoyatangaza na zimtangaze mara
moja Lowassa kuwa ni mshindi wa nafasi ya urais na Duni Juma Haji kuwa
Makamu wa Rais,” walisema viongozi hao.
0 comments:
Post a Comment