Mbunge
wa Ilala jijini Dar es Salaam,Musa Hassan Zungu (katikati) pamoja na
Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao (wapili kushoto)
wakikata utepe kuzindua duka jipya la kutoa huduma mbalimbali za Vodacom
Tanzania lililopo barabara ya Uhuru Kariakoo,wengine katika picha
kushoto ni Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo,Rosalynn
Mworia na Mteja wa kwanza kufika katika duka hilo,Abdulqadir Rashidi.
Mbunge
wa Ilala jijini Dar es Salaam,Musa Hassan Zungu(kulia)akisisitiza jambo
kwa Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao(watatu toka
kushoto)wakati wa uzinduzi wa duka jipya la kutoa huduma mbalimbali za
Vodacom Tanzania lililopo barabara ya uhuru kariakoo,wengine katika
picha wa kwanza kushoto ni Ofisa mkuu wa mauzo na Usambazaji Keith Tukei
na Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo,Rosalynn Mworia.
Mbunge
wa Ilala jijini Dar es Salaam,Musa Hassan Zungu(kulia)akimsikiliza
jambo Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao(watatu toka
kushoto)wakati wa uzinduzi wa duka jipya la kutoa huduma mbalimbali za
Vodacom Tanzania lililopo Barabara ya Uhuru Kariakoo, wengine katika
picha kushoto ni Ofisa mkuu wa mauzo na Usambazaji Keith Tukei na Mkuu
wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo,Rosalynn Mworia.
Mbunge wa jimbo la Ilala jijini Dar es
Salaam,Mussa Hasan Zungu ameyaasa makampuni yanayotoa huduma za simu
nchini kuzidi kuzidi kubuni huduma za kurahisisha maisha kwa wateja na
kusogeza huduma zaidi kwa wananchi ili wazipate popote walipo.
Zungu aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa duka jipya linalotoa
huduma mbalimbali za Vodacom lililopo barabara ya uhuru Kariakoo katika
mwendelezo wa kampuni hiyo kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja ambapo
imefungua maduka katika sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam na maeneo
mengine nchini. “Nawapongeza kwa kusogeza huduma hasa katika kipindi
hiki ambacho sekta ya mawasiliano inazidi kukua siku hadi siku”alisemaMkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao alisema kuwa kampuni imejipanga kuendelea kuboresha huduma zake na kuwekeza zaidi katika kuimarisha huduma ili kuwawezesha wananchi na wateja kwa ujumla kuzipata kwa urahisi.
“Sisi kama kampuni tunaamini kuwa tumefikia mahali tulipo kutokana na wateja wetu kutuamini na kuendelea kutuunga mkono na ndio maana nasi tumeamua kutumia kipindi hiki kuwasikiliza vilevile kuwasogezea huduma karibu na kwa mara nyingine napenda kusema Ahsante wateja wetu waliopo katika mtandao wetu na wale ambao hawajajiunga na mtandao wetu tunawakaribisha wajiunge ili waendelee kupata huduma bora”Alisema.
Ferrao alizitaja baadhi ya huduma za kampuni hiyo ambazo zinaendelea kurahishisha maisha kuwa ni M-Mpesa ambayo inategemewa na makampuni na watu binafsi kutuma fedha na kufanya mihamala mbalimbali ya malipo kwa hapa nchini na ikiwa tayari imevuka mipaka ya nchi bila kusahau huduma ya Kilimo Klub ambayo imelenga kuwakwamua wakulima na kuwarahisisha maisha na huduma ya kutoa mikopo nafuu ya M-PAWA vilevile alitangaza kuzinduliwa kwa kifurushi kipya kinachojulikana kama Mpango mzima ambacho kinatoa unafuu kwa wateja kupata huduma za data.
Baadhi ya wateja waliohudhuria hafla ya uzinduzi huo walisifu hatua ya Vodacom kuzindi kusogeza huduma karibu na wananchi “Huduma hizi zikisogea karibu nasi zinatupunguzia adha ya kutembea muda mrefu kuzifuata nawapongeza Vodacom kwa kuwajali wateja wake”.Alisema Abdulqadir Rashid mmoja wa wateja aliyefika dukani hapo.
Tofauti na mwaka jana ambao kampuni ya Vodacom iliadhimisha wiki ya huduma kwa wafanyakazi wake kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii,mwaka huu wafanyakazi na maofisa wa kampuni wameweza kukutana na wateja na kuwaelimisha huduma mbalimbali za kampuni ikiwemo kusogeza huduma karibu kwa wateja kwa kufungua maduka sehemu mbalimbali jijini Dar es salaam na Masasi mkoani Mtwara.
Katika mkoa wa dar es Salaam maduka ya Vodacom yamefunguliwa katika sehemu za Ubungo,Mbezi Beach,Mbweni na kariakoo.Vodacom ina mtandao wa maduka ya kutoa huduma kwa wateja zaidi ya 100 kwa nchi nzima.
0 comments:
Post a Comment