Dar es Salaam, Novemba 09, 2015: Kampuni ya simu ya Tigo imeomba radhi wateja wake kutokana na
kukatika kwa huduma zake katika sehemu nyingine nchini jana.
Taarifa ya
kampuni hiyo iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam imesema
kukatika kwa huduma za Tigo “kulitokana na sababu zilizo nje ya uwezo kwa kampuni
zilizo tokana na kukatika kwa mkongo sehemu tofauti tofauti.” Aidha taarifa hiyo
iliendelea kusema kwamba “tatizo hilo sasa limeshughulikiwa kikamilifu na huduma
zote za Tigo zimerejea katika hali yake ya kawaida.’’
“Tuna sikitishwa
na usumbufu uliojitokeza kutokana na kukatika kwa huduma zetu natunapenda kuwahakikishia
wateja wetu dhamira ya kampuni yetu kuendelea kuwapa wateja huduma zenye ubora wa
hali ya juu, za kutegemewa na kwa gharama nafuu,” amesema Meneja Mkuu wa Tigo,
Diego Gutierrez.
Aidha Gutierrez
ametoa shukrani kwa wateja wa Tigo kwa uvumilivu wao na kutangaza kwamba kama ishara
ya kuomba msamaha kampuni ina wapa wateja wake wote dakika 10 za muda wa maongezi,
SMS za bure kwenda mtandao yote na 10mb za kuperuzi Intaneti kwa siku nzima ya leo.Kifurushi
hiki mteja ana kipata kwa kutuma neno BURE kwenda namba 15304.
Mwisho
Kuhusu Tigo:
Tigo ni kampuni ya mawasiliano ya
simu za mikononi yenye ubunifu mkubwa nchini Tanzania , ikijulikana kama “nembo
ya maisha ya kidijitale yanayojitosheleza”. Inatoa huduma mbalimbali kuanzia
huduma ya sauti, ujumbe mfupi, intaneti yenye kasi na huduma za kifedha za
kwenye mitandao ya simu za mikononi, Tigo imeanzisha ubunifu kama vile Facebook
ya Kiswahili, Kiunga cha Tigo Pesa kwa watumiaji wa simu za Android & iOS,
Tigo Music( Deezer)na huduma ya kwanza Afrika Mashariki kutuma fedha kwa njia
ya simu za mikononi nje ya nchi yenye uwezo wa kubadili sarafu ya nchi husika.
Intaneti ya Tigo ya 3G inatoa huduma bora kwa
wateja wake katika mikoa yote nchi nzima, na hivi karibuni tumezindua mtandao wa 4G ambao kwa sasa unapatikana Dar
es Salaam nzima,na tunatarajia kuzindua nchi nzima. Kati ya mwaka 2013
na mwaka 2014 pekee kampuni ilizindua zaidi ya maeneo mapya 500 yenye mtandao
wa Tigo na kufanya kuwa zaidi ya maeneo 2000 ya mtandao na inapanga kuongeza
uwekezaji wake mara mbili ifikapo 2017 katika suala la upatikanaji wa mtandao
na kuongeza uwezo wa upatikanaji wa mtandao kwa maeneo yasiyofikika kabisa
vijijini. Pamoja na kuwa na zaidi ya wateja milioni 9 waliosajiliwa, Tigo
imeajiri zaidi ya watanzania 300,000 ikiwa ni pamoja na mtandao wa wawakilishi
wa huduma kwa wateja, wafanyabiashara wakubwa wa fedha za kwenye simu za
mikononi, mawakala wa mauzo na wasambazaji.
Tigo ni nembo kubwa ya kibiashara ya kampuni
la Millicom, kampuni ya kimataifa inayoendeleza maisha ya kidijitale katika
nchi 11 pamoja na shughuli za kibiashara katika Afrika na amerika ya Kusini na
ina ofisi kubwa Ulaya na Marekani. Pamoja na ujuzi Fulani walionao ambao
unawafanya kubuni mara kwa mara na kuwafanya wawe juu, Millicom anaendelea
kujenga thamani kubwa kwa mbia; kutumia dhana yao ya "mahitaji zaidi" hivi ndivyo wanafanya biashara na kurejesha
nafasi yao kama viongozi wa maisha ya kidijitale hasa katika masoko zaidi ya
kipekee na yenye changamoto.
John Wanyancha – Meneja
Mawasiliano
Mobile:
0658 123 089
0 comments:
Post a Comment