Baada
ya kumsimamisha kwa muda usiojulikana, hatimaye uongozi wa Yanga
umetangza rasmi kuvunja mkataba na kiungo wake wa kimataifa kutoka
Rwanda Haruna Niyonzima.
December 28, 2015, mkuu wa idara ya Habari wa klabu hiyo Jerry Muro, alizitaja sababu kubwa za klabu hiyo kufikia uamuzi huo.
“Mchezaji
huyu amekuwa akichelewa na kukosekana mara kwa mara kwenye program za
timu hususan anapokuwa amekwenda kwenye timu yake ya taifa ya Rwanda na
pia kipindi ambacho mchezaji huyu amekuwa akienda likizo. Mara zote
alipokuwa akiitwa na timu yake ya taifa amekuwa akiondoka bila kuomba
ruhusa wala klabu kujua. Amekuwa akishiriki kwenye mashindano ambayo si
rasmi na bila kuruhusiwa na klabu”, amesema Muro.
Mbali
na kuvunja mkataba na Niyonzima, Muro ameeleza pia hatua zaidi
zilizochukuliwa dhidi ya mchezaji huyo kipenzi cha wanajangwani.
“Klabu
pia inamtaka Haruna Niyonzima kulipa fidia ya jumla ya dola za
kimarekani 71, 175 hii ikiwa ni kufidia gharama ambazo Yanga imeingia
katika kumuongezea mkata wake mpya ambao unamalizika mwaka 2017 “,
aliongeza Muro.
Timu ya ushindi imepiga story na Niyonzima kutaka kujua hatma yake baada ya klabu yake kutangaza kuvunja mkata dhidi yake.
“Nimesikia
tu kwa watu, lakini si sahihi kwasababu inavyotakiwa natakiwa kujua
kupitia barua, lakini bado sijapata barua siwezi kulizungumzia hilo”,
alisema Niyonzima wakati akizungumza na Hahaya Mohamed.
Mtandao
huu haukuishia hapo tu, bali ulitaka kufahamu pia mashabiki na
wanachama wa klabu hiyo kutaka kujua wanamaoni gani baada ya klabu yao
kutangaza imesitisha mkataba na Haruna Niyonzima.
“Niyonzima
ni mchezaji mzuri, tulikuwa tunampenda lakini ana mambo yake hata sisi
tulikuwa haturidhiki nayo. Kwasababu kama umeajiliwa lazima uitumikie
kazi sasa wewe kama unaiona kazi haikufai basi tafuta sehemu nyingine”,
alisema mmoja wa wanachama wakongwe wa klabu hiyo.
Awali
klabu ya Yanga ilitanga kumsimamisha Haruna Niyonzima kwa kuchelewa
kuripoti kambini baada ya kuitumikia timu yake ya taifa kwenye michuano
ya Challenge Cup na kushindwa kutoa maelezo kwa kina baada ya kutakiwa
kufanya hivyo.
Hapa
chini unaweza kujionsea video wakati Niyonzima akitoa majibu yake
alipoulizwa kama anataarifa juu ya kuvunjwa kwa mkataba kati yake na
Yanga.
0 comments:
Post a Comment