Thursday, December 24, 2015
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, SACP Justus Kamugisha.
ASKARI
Polisi wa Kituo cha Polisi Nyamagana jijini Mwanza, Konstebo Daud
Masunga Elisha, amemuua askari mwenzake, Konstebo Petro Saimon Matiko
kwa risasi na baadaye kujiua kwa risasi na kufa papo hapo.
Tukio
hilo lilitokea jana saa 8.30 mchana jijini Mwanza katika eneo la Benki
ya Posta Tawi la Pamba wilayani Nyamagana huku chanzo cha mauaji hayo
kikiwa hakijulikani.
Akizungumzia
tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Justus Kamugisha alisema
kitendo hicho si cha kawaida ndani ya jeshi hilo, na kufafanua jinsi
mazingira ya tukio lilivyotokea na kusababisha taharuki kwa wananchi na
wateja waliokuwa ndani na nje ya benki hiyo.
“Ni
kweli kuna askari wawili wamefariki eneo la Benki ya Posta. Katika eneo
la benki hiyo kulikuwa na askari wawili waliokuwa lindoni ambao ni PC
Elisha na PC Remigius Alphonce mwenye namba H 4291, wakiwa wanaendelea
na lindo alifika askari mwingine aliyekuwa amevaa kiraia PC Matiko na
kuwasalimia kisha kuingia ndani ya benki kuchukua fedha,” alieleza Kamanda Kamugisha na kuongeza:
“Baada
ya dakika tano, Matiko alitoka nje na kuwaeleza askari wenzake kwamba
mtandao unasumbua, wakati akieleza hivyo, ghafla askari PC Elisha
aliweka chemba risasi ambapo mwenzake PC Alphonce alimhoji mbona unaweka
risasi katika hali ya utayari wa kutumika na alijibiwa kwa ufupi kwamba
‘achana na mimi.’
“Ghafla
alimfyatulia risasi PC Matiko na kumpiga eneo la bega la kushoto na
kutokeza mgongoni na kuanguka chini, kitendo hicho kilimfanya PC
Alphonce kukimbilia Benki ya Barclays ili kuomba msaada kwa askari
wenzake waliokuwapo lindoni hapo.
“Kabla
ya askari hao kufika, ilisikika sauti ya mlio wa risasi na baada ya
kurudi alimkuta PC Elisha akiwa amejipiga risasi kwenye paji la uso na
kutokea nyuma ya kisogo, tayari akiwa amepoteza maisha.”
Mpekuzi blog
0 comments:
Post a Comment