Kupinduka na Kuwaka Moto
Mpekuzi blog
WATU
saba wamefariki duniani na wengine kumi wamejeruhiwa katika ajali ya
gari walilokuwa wakisafiria kupinduka na kulipuka na kuwaka moto.
Akiongea
na mtandao huu ofisini kwake Mganga Mkuu wa hospitali ya Mkoa wa Kigoma
Maweni Dkt. Leonard Subi amesema kuwa jana majira ya saa 12 jioni
walipokea miili ya marehemu 6 na majeruhi 11 ilipofika saa 6 usiku
majeruhi mmoja alifariki duniana na kupelekea idadi ya vifo kuwa saba.
Aliwataja
waliofariki katika ajali hiyo ni Ashura Mussa, Kadogo Yusuph, Kabwe
Iddy, Mwamvua Juma na Peter Sungura,maremu wawili miili yao bado
haijatambulika sababu ya kuungua vibaya.
Dkt.
Subi aliwataja pia majeruhi wa ajali hiyo kuwa ni Andrew Peter, Amos
Thomas, Mutta Hamis, Shabaan Fadhil, Hassan Kasa, Esau Elias, Asha
Kassim na Riziki Jaah.
"Majeruhi
wote wamelazwa wodi namba saba na hali zao siyo nzuri wanaendelea na
matibabu, mtoto aitwaye Riziki Jaah mwenye umri wa miezi nane ndiye
aliyenusurika katika ajali hiyo hajaumia popote mama yake alimtupa
dirishani baada ya moto kuwaka ila mama yake alifariki kwa kuungua
kwenye ajali hiyo"alisema Dkt. Subi.
Naye
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kigoma, Ferdnand Mtui amethibitisha
kutokea kwa ajali hiyo ya gari aina ya Toyota Hiace lenye namba T.700
ADK lililokuwa likitoka Kigoma mjini kwenda katika kijiji cha Subankala
kata ya Ilagala Wilayani Uvinza kilichopo mwambao mwa ziwa Tanganyika.
Kamanda
Mtui alisema kuwa ajali hiyo ilitokea katika kijiji cha Mwakizega na
chanzo cha ajali hiyo ni dereva kuwakwepa watembea kwa miguu kisha
kugonga gema iliyopelekea gari kupinduka na kuwaka moto.
0 comments:
Post a Comment